Jina la filamu ijayo ya Star Wars latangazwa

Jina la filamu mpya ya mwendelezo wa filamu za Star Wars limetangazwa, ambapo itaitwa Star Wars: The Last Jedi.
Katika taarifa kwenye mtandao wa Star Wars, watunga filamu hizo wamesema wako na mashabiki sugu wa filamu hizo na hata filamu nyingine na walitaka wawe wa kwanza kufahamu jina hilo.
''Kwa kuwashukuru mashabiki wetu, tunataka kuwafahamisha kwanza jina la sura inayofuata ya hadithi ya Skywalker ambayo itaitwa: STAR WARS: THE LAST JEDI.''
Makala ya 8 ya filamu hizo, - The Last Jedi - itazinduliwa rasmi mwezi Desemba.

Chanzo cha picha, Jonathan Olley/Lucasfilm
Hakuna tole fupi la kuvumisha filamu hiyo lililotolewa kufikia sasa, lakini rais wa Lucasfilm Kathleen Kenndy, amedokeza kutakuwa na tangazo hilo katika majira yajayo ya kuchipua.
Watakaoigiza ni Daisy Ridley, John Boyega, Oscar Isaac, Anthony Daniels na Lupita Nyong'o .
Pia itamjumuisha hayati Carrie Fisher, kwani filamu hiyo ilikamilika mwaka jana kabla ya kifo chake .

Chanzo cha picha, Jonathan Olley/Lucasfilm
Filamu hiyo ya Last Jedi iliandikwa na kuelekezwa na Rian Johnson na maprodusa ni Kathleen Kennedy na Ram Bergman.
Wazalishaji wake wakuu ni J.J. Abrams, Jason McGatlin na Tom Karnowski.













