Watalii waondolewa Gambia

Chanzo cha picha, PA
Maelfu ya watalii wanaondolewa nchini Gambia ,ambapo rais Yahya Jammeh amekataa kujiuzulu na ametangaza hali ya tahadhari ya siku 90.
Serikali za magharibi mwa Afrika zimeonya uwezekano wa kuzuka kwa ghasia na zimewataka raia kutoelekea katika taifa hilo.
Bw Jammeh anatarajiwa kukabidhi mamlaka siku ya Alhamisi kwa kiongozi wa upinzani Adama Barrow, aliyeshinda uchaguzi mwezi Disemba.

Mataifa ya Magharibi mwa Afrika yamemtaka rais huyo aliyeshindwa katika uchaguzi kung'atuka mamlakani na wanajiandaa kutekeleza uvamizi wa kijeshi iwapo ataendelea kukataa.








