Adama Barrow apewa makao Senegal

Rais wa Senegal Macky Sall, amekubali kumpa makao bwana Barrow kwenye mji mkuu Dakar

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Rais wa Senegal Macky Sall, amekubali kumpa makao bwana Barrow kwenye mji mkuu Dakar

Ripoti kutoka chini Senegal zinasema kuwa rais mteule wa Gambia Adama Barrow atasalia nchini Senegal hadi wakati wa kuapishwa kwake wakati huu ambapo nchi ya Gambia inakumbwa na mzozo.

Shirika la habari nchini Senegal linasema kuwa rais wa nchi hiyo Macky Sall, amekubali kumpa makao bwana Barrow kwenye mji mkuu Dakar hadi pale atakapoapishwa tarehe 19 mwezi huu.

Rais wa sasa Yahya Jammeh amekataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba.

Siku ya Jumamosi rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita, alimtaka rais wa Gambia kuondoka madarakani ili kuzuia kuzuia umwagaji damu.

Alikuwa akizungumza wakati wa mkutano Afrika na Ufaransa kwenye mji mkuu wa Mali, Bamako, ambao ulitawaliwa na mzozo ulio nchini Gambia.

Rais wa sasa Yahya Jammeh amekataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Rais wa sasa Yahya Jammeh amekataa kukubali kuwa alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba