Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Maelfu wahudhuria mazishi ya Rafsanjani
Maelfu ya watu nchini Iran wamejitokeza kwenye mji mkuu Tehran kwa mazishi ya rais wa zamani Akbar Hashemi Rafsanjani.
Kiongozi wa Iran Ayatollah Ali Khamenei aliongoza maombi kwenye sherehe hizo.
Rafsanjani ambaye alikuwa rais kati ya mwaka 1989 na 1997 aliaga dunia kutoka na mshutuko wa moyo siku ya Jumapili akiwa na umri wa maika 82.
Alikuwa mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa tangu yafanyike mapinduzi ya mwaka 1979.
Televisheni ilionyesha umati mkubwa wa waombolezaji katika mitaa inayozunguka chuo kikuu cha Tehran ambapo maombi yanafanyika.