Chanjo ya Ebola yafanikiwa

Watu 6000waliopata chanjo hiyo, walionekana kuwa bila ugonjwa huyo siku kumi baadaye.

Chanzo cha picha, CDC/SCIENCE PHOTO LIBRARY

Maelezo ya picha, Watu 6000waliopata chanjo hiyo, walionekana kuwa bila ugonjwa huyo siku kumi baadaye.

Majaribio ya chanjo cha ugonjwa wa Ebola yamebainika kuwa yana uwezo na nguvu zaidi dhidi ya virusi vya ugonjwa huo hatari.

Majaribio yake yamefanyiwa nchini Guinea, mojawepo ya mataifa ya Afrika magharibi ambayo yalikumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo, ambao ulimalizika mwaka huu.

Matokeo ya mwisho ya majaribio hayo, yaliyochapishwa kwenye jarida la maswala ya matibabu linalochapishwa nchini Uingereza, The Lancet, yanaonyesha kuwa takriban watu elfu sita waliopata chanjo hiyo, walionekana kuwa bila ugonjwa huyo siku kumi baadaye.

Miongoni mwa kundi lingine kama hilo, ambao hawakupewa chanjo, watu 23 walipatikana na virusi vya Ebola.

Mkurugenzi mkuu wa taasisi moja ya matibabu nchini Uingereza- Wellcome Trust, ameelezea matokeo hayo kama ya kufana mno.

Watu elfu 11 walifariki wakati wa mliouko wa hivi majuzi wa ugonjwa wa Ebola afrika magharibi.

Watu 11,000 walifariki wakati wa mlipuko wawa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi.

Chanzo cha picha, CDC/SCIENCE PHOTO LIBRARY

Maelezo ya picha, Watu 11,000 walifariki wakati wa mlipuko wawa ugonjwa wa Ebola Afrika Magharibi.