Kanye West bado atawania urais 2020?

Kanye

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kanye West alitangaza mwaka jana kwamba atawania urais 2020

Kanye West amelejea kwenye Twitter na inaonekana kana kwamba ameamua kuchelewesha nia yake ya kuwania urais Marekani.

Mwanamuziki huyo alikuwa hajaandika ujumbwe wowote kwenye mitandao ya kijamii tangu alipolazwa hospitalini mwezi uliopita.

Kanye aliandika kwenye Twitter kufafanua yaliyojiri kwenye mkutano wake na Donald Trump, ambapo alisema walikutana "kujadili masuala mengi yanayoangazia tamaduni nyingi."

Mwishoni kabisa, aliandika "#2024".

Wengi wanaamini alikuwa anagusia mpango wake wa kutaka kuwania urais Marekani.

Alitangaza nia yake mara ya kwanza wakati wa tuzo za video za muziki za MTV mwaka 2015.

Wakati huo, alisema angewania 2020.

Lakini baadhi sasa wanasema ameahirisha mpango wake ili kumpa Trump fursa ya kuwania uras kwa muhula wa pili.

Kanye West majuzi alitangaza kwamba iwapo angepiga kura mwaka huu basi angempigia Bw Trump.

Donald Trump na Kanye West

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kanye West alipokutana na Trump katika jumba la Trump Tower jijini New York

Bw Trump alipokutana na Kanye Jumanne alisema wao ni "marafiki" na kumweleza Kanye kama "mtu mzuri".