Koeman amkejeli Wenger kwa kumlaumu refa

Ushindi mara mbili wa Koeman dhdi ya Wenger ulikuwa wakati alikuwa akiongozoa klabu ya Southampton

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Ushindi mara mbili wa Koeman dhdi ya Wenger ulikuwa wakati alikuwa akiongozoa klabu ya Southampton

Meneja wa Everton Ronald Koeman amemkejeli Arsene Wenger kwa kulalamikia uamuzi wa refa Mark Clattenburg, baada ya Everton kuishinda Arsenal kwa mabao 2-1.

Wenger alihisi kwa kuna ambayo ilichangia ushindi wa Everton haikuwa sahihi.

Siwezi kushangaa kwa sababu hii ni mara ya tatu mfululizo nimeshinda dhidi ya Arsenal na mara ya tatu mfululizo refa amelaumiwa.

Everton wamepata pointi nyingi kutoka kwa timu zinazopoteza

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Everton wamepata pointi nyingi kutoka kwa timu zinazopoteza

Ushindi mara mbili Koeman alipata dhidi ya Arsenal, aliupata wakati akiongozo klabu ya Southampton ambayo ilishinda kwa mabao 4-0 mwezi Desemba mwaka 2015 na kwa mabao 2-0 miezi 11 baadaye.

Arsenal inasalia ya pili katika ligi kuu, pointi tatu nyuma na Chelesea, na ushindi huo wa Everton ulifikisha mechi ya tano ambapo Arsenal haijapata ushindi.

Wenger amefeli kumshinda Koeman katika mechi nne zilizopita.