Indonesia: Tetemeko labomoa majumba na kuua watu wengi

Mnara wa msikiti eneo la Pidie, Indonesia

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Majumba kadha, ikiwemo misikiti, yameporomoka

Tetemeko kubwa la ardhi limeua watu zaidi ya 24 na kusababisha uharibifu mkubwa katika mkoa wa Aceh nchini Indonesia.

Maafisa wanasema watu wengi wamefukiwa kwenye vifusi vya majumba yaliyoporomoka.

Tetemeko hilo la nguvu ya 6.4 kwenye vipimo vya Richter lilitokea karibu na mji wa Sigli katika kisiwa cha Sumatra ambapo majumba mengi yameporomoka.

Shirika la utabiri wa hali ya hewa la Indonesia limesema hakuna hatari ya kutokea kwa kimbunga.

Mwaka 2004, mkoa wa Aceh uliathiriwa sana na kimbunga kilichosababishwa na tetemeko kubwa baharini. Watu 120,000 waliuawa mkoani humo.

Taasisi ya Jiolojia ya Marekani imesema tetemeko hilo lilitokea karibu na pwani mwendo wa saa 11:03 asubuhi saa za huko (22:03 GMT Jumanne) katika kina cha 17.2km (maili 11) chini ya ardhi.

Said Mulyadi, naibu mkuu wa wilaya ya Pidie Jaya, eneo lililoathiriwa pakubwa na tetemeko hilo, ameambia idhaa ya BBC ya Indonesia kwamba huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka.

Maafisa wamesema huenda kusitokee kimbunga

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Maafisa wamesema huenda kusitokee kimbunga
Map of Indonesia
Vifusi vya jumba mkoani Aceh tarehe 7 Desemba 2016.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Maafisa wa uokoaji wanawatafuta manusura
Vifusi vya jumba Pidie, Indonesia Sumatra, Desemba 7, 2016.

Chanzo cha picha, AFP/Getty Images

Maelezo ya picha, Maafisa wanahofia huenda idadi ya waliofariki ikaongezeka kwani watu wengi wamefukiwa kwenye vifusi vya majumba yaliyobomoka