Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kuzaa kwa upasuaji kunaokoa maisha
Wanasayansi duniani wanasema kujifungua mtoto kwa njiya ya upasuaji kunaimarisha maumbile.
Wanawake wengi wanajifungua watoto kwa njia ya upasuaji kwa sababu njia ya kizazi ni nyembamba.
Kabla ya njiya hii kuanza, wanawake wengi walifariki dunia wakati wa kujifungua.
Wanasayansi kutoka Austria wanasema vifo vya wanawake wakati wa kujifungua vimepunguzwa kwa sababu ya upasuaji.
Hata hivyo imegunduliwa kwamba mwanamke aliye na njia nyembamba ya kizazi huenda pia mwanawe wa kika akarithi hali sawa na yake.
Watafiti wanasema visa vya watoto kushindwa kuzaliwa kwa njia ya kawaida vimeongezeka kwa kati ya asili mia 10 na 20.
Utafiti huu umechapishwa na jarida Taasisi ya 'National Academy of Sciences'.