Maelfu waandamana wakimtaka rais wa Korea Kusini ajiuzulu

Chanzo cha picha, Reuters
Maelfu ya watu nchini Korea Kusini wamekusanyika kwenye mji mkuu Seoul kwa wiki ya sita mfululizo wakitaka rais Park Geun-hye ajiuzulu.
Maandamano ya hivi punde yanajiri muda mfupi baada ya vyama vya upinzani kupeleka bungeni mswada wa kumuondoa madarakani Rais Park.
Mswada huo unaoungwa mkono na wabunge 170 unapigiwa kura wiki ijayo.

Chanzo cha picha, AFP
Rais Park amesema kuwa ana nia ya kuondoka madarakani kufuati madai kuwa walishirikiana na rafiki wake wa karibu Choi Soon-sil, ambaye anakabiliwa na mashataka ya ufisadi.








