Mtandao wa uhamiaji wa Canada wakumbwa na tatizo

Mtandao wa idara ya uhamiaji nchini Canada umekumbwa na matatizo ambayo yamesababisha usitumike wakati wa uchaguzi wa urais nchini Marekani.
Hali hiyo imesababisha kuenea uvumi kuwa tatizo hilo limetokana na watu wengi wanatembelea mtandao huo kutoka nchini Marekani kufuatia ushindi wa Donald Trump kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani.
Maafisa kutoka idara ya uhamiaji nchini Canada hawangeweza kupatikana kujibu madai hayo lakini wataalamu wanasema kuwa tatizo hilo huenda limesababishwa na sababu zingine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Hilo si tatizo pekee linalohusishwa na uchaguzi wa Marekani.
Maafisa walishindwa kuingia kwenye mtandao wa uchaguzi katika jimbo la Colorado kwa muda wa nusu saa hivi siku ya Jumanne alasiri
Pia bodi ya uchaguzi katika jimbo la North Carolina, ililazimika kuacha kutumia mfumo wa eletroniki kupiga kura, na kutumia makaratasi baada ya kukumbwa na hitilafu za kiufundi.








