Meya auawa korokoroni Ufilipino

Meya Espinosa (kushoto) alijisalimisha kwa polisi mwezi Agosti

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Meya Espinosa (kushoto) alijisalimisha kwa polisi mwezi Agosti

Meya mmoja nchini Ufilipino ambaye alizuiliwa kwa kushiriki kwenye ulanguzi wa madawa ya kulevya ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa korokoroni.

Polisi wanasema kuwa Rolando Espinosa ambaye ni meya wa mji wa Albuera aliuawa akiwa na mfungwa mwenzake baada ya kuwafyatulia polisi risasi walipokuwa wakifanya msako kutafuta silaha haramu.

Bwana Espinosa ni mmoja wa maafisa zaidi ya 150 waliotajwa mwezi Agosti na rais Rodrigo Duterte, kama sehemu ya kampeni ya kuwaweka hadharani wale wanaoshiriki biashara ya madawa ya kulevya. Alikuwa amejisalimisha akidai kuwa alihofia maisha yake

Sera za Rais Duterte za kupambana na madawa ya kulevya zimepigwa vikali

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Sera za Rais Duterte za kupambana na madawa ya kulevya zimepigwa vikali

Wiki iliyopita meya mwingine ambaye alitajwa na Duterte aliuawa wakati wa ufyatuliaji wa risasi na polisi kusini mwa ufilipino.