Wachezaji wanaotumia lugha ya Lingala kuchanganya walinzi

Chanzo cha picha, Getty Images
Wachezaji wa Everton Romelu Lukaku na Yannick Bolasie, ambao wametajwa kuwa washambuliaji walio na ushirikiano mkubwa zaidi, wakiwa wamefunga mabao manane kwa kushirikiana msimu huu, wamefichua kuwa asili yao ambayo ni Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ndiyo imechangia mafanikio yao.
Bolasie aliambia gazeti la Liverpool Echo kuwa, wao huwasiliana kwa lugha ya Lingala ili kuwachanganya walinzi ambao wanajaribu kupima mienendo yao.
"Hamna walinzi wengi wanaofahamu lugha ya Lingala kwa hivyo hilo hutupatia fursa nzuri," alisema Bolassie.

Chanzo cha picha, AFP
Lukalu ni raia wa Ubelgiji lakini wazazi wake ni raia wa Congo huku Bolasie huchezea timua ya taifa ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
Huu ni mfano wa lugha ambayo wachezaji hao hutumia uwanjani jinsi ivyotafsiriwa na Mila Kimbuni kutoka Jamhuri ya Demokrasi ya Congo ambapo lugha hiyo hutumiwa sana.
Weka mpira eneo la hatarai - "Tinda N'ango cote oyo!"
Weka kwa kichwa- "Mutu"
Songa mbele- "Landa nzela"
Shambulia- "Marquer nbala moko"
Moja mbili- "Zongisela Nga Ango"












