Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Jumba la Adolf Hitler sasa kutobomolewa
Serikali ya Austria imesitisha mpango wake wa kutaka kubomoa nyumba ambazo Adolf Hitler alizaliwa,baada ya jopo la wataalam kusema kuwa halikuwa pendekezo lao.
Waziri wa maswala ya ndani ,Wolfgang Sobotka alitangaza jana kwamba jengo jipya litajengwa mahala hapo.
Lakini katika taarifa yake siku ya Jumanne, sasa ameunga mkono pendekezo hilo la wataalam kwamba kulibadilisha jumba hilo na kulifanya kuwa la serikali ama kitu chochote kinachokaribia hilo kutaathiri kumbukumbu zake.
Limekuwa jumba la kuhiji la watu wa Nazi.
Wataalam hao wamesema kuwa kubomolewa kwa jengo hilo kutaharibu kumbukumbu za watu wa Nazi.