Matokeo ya Bara la Afrika kufuzu kombe la dunia

Chanzo cha picha, EPA
Barani Afrika kumepigwa michezo minne ya kuwania kufuzu kwa fainali za kombe la dunia zitazofanyika nchini Urusi Mwaka 2018.
Nigeria Super Eagle wakicheza ugenini wamewatambia wenyeji wao Zambia chipolopolo kwa kuiwachapa kwa mabao 2-1.
Mabao ya Nigeria yakifungwa na Alex Iwobi na Kelechi Iheanacho, goli la Zambia likifungwa na Collins Mbesuma
Algeria wakicheza katika uwanja wao wa nyumbani wametoshana nguvu na Cameroon kwa kufungana bao 1-1.
Mafarao Misri wamewatambia Congo kwa kuwachapa kwa mabo 2-1 huku Tunisia nao wakishinda nyumbani kwa mabao 2 - 0 dhidi ya Guinea.








