Vyoo vilivyojengwa kwa vioo vyazinduliwa nchini China

Chanzo cha picha, Barcroft
China imezidisha matumizi yake ya vioo kuunda vivutio vya kitalii kwa kujenga choo cha vioo ambacho mtu anaweza akaona nje na hata ndani.
Vyoo hivyo, vimejengwa karibu na Ziwa Shiyan, katika mkoa wa Hunan kusini mwa nchi hiyo.
Vioo hivyo vinawezesha wanaovitumia vyoo hivyo kutazama mandhari ya kuvutia ya msitu au wengine wanaotumia vyoo jirani.
Aidha, walio nje wanaweza kuona walio ndani ya vyoo.
Kuta za vyoo hivyo, hata zile zinazotenganisha vyoo vya wanawake na wanaume, ni za vioo kabisa ingawa vioo hivyo vimetiwa ukungu kiasi.
Vyombo vya habari nchini humo vinasema ni watu wachache sana waliotumia vyoo hivyo siku ya kuzinduliwa kwake.

Chanzo cha picha, Barcroft Images
Licha ya umaarufu wa mijengo ya kutumia vioo katika ujenzi, hasa kwenye madaraja na barabara, baadhi ya miradi imefungwa.

Chanzo cha picha, Barcroft

Chanzo cha picha, Barcroft
Habari za kuzinduliwa kwa vyoo hivyo zimevuma sana.
Ejike Nnadi, akichangia ujumbe wa Facebook wa runinga ya taifa CCTV amesema: "Hapana".
Lakini kunao wengine wanaosema wanaweza kujaribu kuvitumia.

Chanzo cha picha, Barcroft
Tina Chen anasema mradi huo wa vyoo ni ishara kwamba kuna mtu alikuwa na pesa za "kupoteza".

Chanzo cha picha, Getty Images














