Madereva wa malori kutoka Tanzania na Kenya waokolewa DRC

Mara nyingi bidhaa husafirishwa kwende DRC kutoka mataifa jirani kwa njia ya barabara

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mara nyingi bidhaa husafirishwa kwende DRC kutoka mataifa jirani kwa njia ya barabara

Madereva nane wa malori kutoka nchini Tanzania na wengine wanne kutoka Kenya wameokolewa baada ya kushikwa mateka mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Madereva hao walitekwa nyara katika mkoa ulio kusini wa Kivu siku ya Jumatano.

Malori hayo yalichomwa moto na madereva wake kutekwa nyara
Maelezo ya picha, Malori hayo yalichomwa moto na madereva wake kutekwa nyara

Wizara ya mashauri ya nchi za kigeni nchini Tanzania ilisema kuwa watekaji nyara wao walikuwa wakiitisha fidia ya dola 4,000 kwa kila dereva.

Hata hivyo waziri wa masuala ya ndani nchini Congo Zakwani Salehe, alisema kuwa hakuna fidia iliyolipwa na ni wanajeshi waliowaokoa madereva hao.

Malori hayo yalichomwa moto na madereva wake kutekwa nyara
Maelezo ya picha, Malori hayo yalichomwa moto na madereva wake kutekwa nyara

Aliwataja watekaji hao kama majambazi na haijabainika ikiwa walikuwa na uhusiano na kundi lolote la waasi linaloendesha shughuli zake mashariki mwa Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.

Mwandishi wa BBC aliyeko mjini Bukavu anasema kuwa visa vya utekaji nyara kwa fidia vinazidi kuongezeka.

Malori hayo yalichomwa moto na madereva wake kutekwa nyara
Maelezo ya picha, Malori hayo yalichomwa moto na madereva wake kutekwa nyara