Malori ya Kenya na Tanzania yachomwa moto DRC

Magari 13 ya mizigo yanayotoka Tanzania na Kenya yamechomwa moto

katika vijiji vya Kasebebena na Matete kilometa 30 kutoka mji wa Namoya katika nchi ya

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kulingana na gazeti la Mwananchi nchini Tanzania,Mmiliki wa kampuni ya Simba Logistics inayomiliki magari 10 kati ya yaliyopata kadhia hiyo,

Azim Dewji amesema magari yake manne yameteketea kabisa na mengine sita yameungua

kidogo huku magari mengine matatu kutoka Kenya nayo yakiteketea kabisa.

Gazeti hilo linadai kuwa,Dewji amesema madereva wa magari hayo walitekwa huku wakipewa sharti la

kutaka majeshi ya Tanzania yaliyo katika ulinzi wa amani nchini humo yaondoke ili

wawaachilie.

Mwananchi linasema kuwa ,hata hivyo taarifa ya Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa) iliyopatikana kupitia

mitandao ya jamii ilisema madereva wawili kati yao walitoroka, huku kikiwataka madereva

wengine kutoelekea nchini humo