Majina mashuhuri zaidi ya watoto Uingereza

Mtoto

Chanzo cha picha, Thinkstock

TJina Noah limeingia kwenye orodha ya majina 10 mashuhuri zaidi kwa kupewa watoto wavulana kwa mara ya kwanza, huku Amelia likisalia kuwa jina ambalo wazazi wengi wanawapa watoto wasichana England na Wales, taasisi ya taifa ya Takwimu Uingereza imeonesha.

Jina Oliver ndio linaloongoza upande wa wavulana, likishikilia nafasi ya kwanza tangu 2013 nalo Amelia likiwa juu kwa wasichana tangu 2011. Watoto walioitwa Oliver mwaka 2015 ni 6,941 na Amelia 5,158.

Maafisa wa ONS waliorodhesha majina kando kwa mujibu wa jinsi jina liliandikwa.

Iwapo majina yanayotamwa kwa njia sawa yangewekwa pamoja, basi orodha hiyo huenda ingelikuwa tofauti kidogo.

Mfano ni jina Muhammad ambalo linashikilia nafasi ya 12 likiwa na watoto 3,730.

Kuna wazazi walioandika jina hilo kama Mohammed (2,332) na wengine kama Mohammad (976). Iwapo majina hayo yangejumlishwa, basi jina hilo lingelikuwa katika 10 bora.

Yalikuwepo majina ya kushangaza. Kwa mfano watoto wavulana 17 na wasichana 15 walipewa jina Baby.

Majuzi, utafiti ulionesha karibu sehemu moja kati ya tano ya wazazi Uingereza wanajutia majina waliyowapa watoto wao.

Rocky Balboa na Apollo Creed

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Rocky Balboa na Apollo Creed

Wavulana 35 walipewa jina Rocky, na 21 wakapewa Apollo, labda kutokana na wahusika wakuu wa filamu ya ndondi Rocky Balboa na Apollo Creed.

Wavulana 15 walipewa jina Blue na wengine 14 wakaitwa Ocean. Na kunao 18 walipewa jina Blu.

Kuna jumla ya wavulana 36 ambao watahitajika kujifunza kuandika na kutamka jina lao, Tymoteusz.

Emilia Clarke anayeigiza kama Daenerys katika Games of Thrones

Chanzo cha picha, PA

Maelezo ya picha, Wasichana watano wameitwa Kaleesi

Upande wa wasichana 280 walipewa jina Arya, mmoja wa wahusika wakuu filamu ya Game of Thrones, na wengine 562 wakaitwa Aria, 33 Ariah, 17 Aaria na sita Aariah, jina ambalo huenda ni moja ila likaandikwa tofauti.

Jina Kaleesi, pia kutoka kwa filamu hiyo, lilipewa wasichana watano.

Jina Princess lilipewa wasichana 72, ikikaribia wavulana 77 walioitwa Prince.

The character Maverick played by Tom Cruise Top Gun

Chanzo cha picha, Alamy

Maelezo ya picha, Perhaps boys called Maverick will grow up to become a Top Gun in whatever they do

Takwimu hizo zinaonesha jina Oliver ndilo maarufu zaidi kwa wavulana maeneo yoteb ya Englandisipokuwa London na West Midlands, ambapo jina Muhammad linaongoza.

Jina Muhammad lilipita Oliver eneo la West Midlands mwaka 2014.

line

Majina mashuhuri zaidi 2015

Oliver Reed
Maelezo ya picha, Jina la marehemu Oliver Reed linasalia kuwa maarufu zaidi kupewa wavulana
  • Oliver 6,941
  • Jack 5,371
  • Harry 5,308
  • George 4,869
  • Jacob 4,850
  • Charlie 4,831
  • Noah 4,148
  • William 4,083
  • Thomas 4,075
  • Oscar 4,066
line

Majina maarufu kwa wasichana 2015

Amelia Boynton Robinson

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha, Amelia Boynton Robinson, mwanaharakati mtetezi wa haki za raia Marekani, alifariki mwaka jana akiwa na umri wa miaka 104
  • Amelia 5,158
  • Olivia 4,853
  • Emily 3,893
  • Isla 3,474
  • Ava 3,414
  • Ella 3,028
  • Jessica 2,937
  • Isabella 2,876
  • Mia 2,842
  • Poppy 2,816
line
Rihanna tuzo za MTV Video Awards New York Agosti 2016

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Wasichana kadha pia wamepewa jina la mwanamuziki Rihanna

Wasichana 72 walipewa jina Adele, 39 wakaitwa Paloma, kutokana na mwanamuziki Paloma Faith.

Kulikuwa na wasichana 35 walioitwa Rihanna, na tisa Rhianna.