Uturuki:Kundi la IS linapaswa kutokomezwa kabisa

Chanzo cha picha, AFP
Waziri wa mambo ya nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu amesema kundi la Islamic state linatakiwa kuondolewa kabisa kutoka mikoa ya kaskazini mwa Syria.
Amri hiyo inakuja huku kukiwa na taarifa kwamba majeshi ya Uturuki yanajiandaa kushikilia mji wa mpakani wa Jarablus ambao upo mikononi mwa I-S .
''Tutapigana kuipinga Islamic State na taasisi nyingine za kigaidi mpaka mwisho. Tutaendelea kuunga mkono nchi zote zinazopambana na vikundi hivyo. Kama unavyojua wapiganaji wa upinzani wamefanikiwa kutekeleza mashambulizi kadhaa AL-Rai na mpakani kwetu.
Kwa hakika, mikoa iliyo mipakani lazima iwaondoe kabisa wapiganaji wa IS. Kwa kipindi hiki tutaendelea kutoa ushirikiano ili kuwaondoa wapiganaji wa IS kutoka katika maeneo''
Wanamgambo wa Islamic state wanashutumiwa kutelekeza shambulizi la bomu la kujitoa mhanga lililotokea mwishoni mwa juma lililopita katika mji wa Gaziantep uliopo kusini mwa Uturuki.

Chanzo cha picha, AFP
Shambulizi hilo lililenga harusi iliyokuwa ikiendelea ambapo takribani watu hamsini waliuawa ,wengi wao wakiwa ni watoto.

Chanzo cha picha, AFP








