Kwa Picha: Waafrika wanaoishi India

Mwezi wa Januari mwana huu, mwanafunzi kutoka Tanzania alidhalilishwa kwa kuvuliwa nguo na umati wa watu katika jiji la Bangalore, kusini mwa India, baada ya gari la mwanafunzi kutoka Sudan kumgonga na kumuua mwanamke mmoja eneo hilo.
Mpiga picha Mahesh Shantaram, alishangazwa na kisa hicho na visa kama hivyo kwa Waafrika nchini India na akaanza kuyaangazia maisha ya Waafrika hao.
Shantaram alianza upigaji picha hizo kutoka Bangalore, na hata kwa miji mengine kama vile Jaipur, Delhi na Manipal akiangazia wanafunzi ambao walikuwa wachache .
Msururu wa picha zao ni sehemu mojawepo ya maonyesho yanayoandaliwa na Tasveer.
"Kila picha ina jukumu lake la kuonyesha jinsi Waafrika wanavyoishi nchini India kwa kuweka picha za upweke, hisia ya uadui, na ukosefu wa nafsi," alisema mtaalam wa sanaa Caroline Bertram, katika makala maalum ya maonyesho hayo.
















