Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Fidel Castro asherehekea kutimiza miaka 90 Cuba
Kiongozi mwanamapinduzi wa Cuba Fidel Castro anasherehekea kutimiza miaka 90 tangu kuzaliwa kwake.
Mzee huyo, aliyetawala kisiwa hicho kwa zaidi ya miaka 50, hajaonekana hadharani kwa miezi mingi na bado haijabainika iwapo atajitokeza leo.
Ingawa Cuba imebadilika sana tangu kakake Raul achukue hatamu miaka minane iliyopita, na ushawishi wa Fidel umeshuka, bado anaenziwa sana na raia wengi wa Cuba.
Hakuna hafla yoyote rasmi iliyopangiwa kufanywa, lakini Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, taifa mshirika wa karibu wa Cuba, amewasili Havana kushiriki katika sherehe hizo.
Mtengenezaji sigara maarufu raia wa Cuba ametayarisha msokoto mrefu zaidi wa sigara duniani kwa heshima ya Castro.
Msokoto huo una urefu wa mita 90.