Victor Osimhen: Mshambuliaji wa Nigeria aliyeisaidia Napoli kuwa miamba wa soka ya Italia

Huku wafuasi wa Napoli wakishangilia kwa mara ya kwanza kutwaa taji la Italia katika kipindi cha miaka 33, ni vigumu kusema kwamba mchezaji yeyote amechangia zaidi kupati

kana kwa taji hilo kuliko mshambuliaji wa Nigeria Victor Osimhen.

Huko nyuma mnamo 1990, mfungaji bora wa Gli Azzurri alikuwa Diego Maradona ambaye alifunga mabao 16 katika mechi 28 za Serie A, na kumfanya awe wa tatu kwenye orodha ya ligi msimu huo.

Osimhen, ambaye anacheza soka lake katika uwanja ambao sasa umepewa jina la Maradona, amevuka kiwango hicho kwa urahisi, akifunga mabao 22 katika mechi 27, likiwemo bao muhimu ambalo lilisaidia kutwaa ubingwa katika sare ya 1-1 dhidi ya Udinese.

Kwa sasa anaongoza orodha ya wafungaji wa Serie A, matatu mbele ya mpinzani wake wa karibu, Lautaro Martinez wa Inter Milan.

Pia alichangia mabao matano ya Ligi ya Mabingwa, kabla ya Napoli kuondolewa katika robo fainali ya michuano hiyo na AC Milan.

'Malengo ya kushinda michezo' ni maneno yanayotumika sana katika soka - na bila shaka mabao ya Osimhen yamevutia umakini. Alijiunga na Napoli mwezi Julai mwaka 2020 kwa ada ya takriban €81m, ambayo ni ya juu zaidi kwa mchezaji wa Kiafrika, tetesi za uhamisho wa kila siku sasa unamhusisha na klabu zote kubwa za Ulaya kwa ada kubwa zaidi.

Lakini je, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 ana thamani ya pauni 100?

Victor Osimhen ni nani?

Kupanda kwa Osimhen katika ulingo wa soka ya Ulaya ni jambo ambalo lilitarajiwa.

Aliwahi kuiwakilisha Nigeria kwenye Kombe la Dunia la Vijana walio chini ya umri wa miaka 17 mwaka 2015, ambapo alifunga mabao 10 na kuisaidia Super Eagles kushinda taji la tano,,

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 aliondoka kwenye chuo cha soka cha Ultimate Strikers ya Lagos na kujiunga na Wolfsburg ya Ujerumani. Wakati huo aliifahamisha BBC kwamba amekataa ofa kutoka kwa Arsenal.

Hatua hiyo haikupokelewa vyema nchini Ujerumani - na nyota katika ligi ya Ujerumani, Bundesliga pia haukung'aa kwani alicheza mechi 16 bila kufunga bao.

"Hawakuwa na subira kumwacha mvulana huyo kukua," alisema mshambuliaji wa zamani wa Wolfsburg Jonathan Akpoborie, ambaye alimwona Osimhen akiwasili akiwa kijana chipukizi.

"Alikuwa mtu wa ajabu wakati huo," Mnigeria huyo aliiambia BBC Sport Afrika.

"Kweli amekuwa na anaendelea vizuri sana. Lakini hatuwezi kuanza kufanya maamuzi kwa sababu amefunga mabao 100.

"Kila mtu sasa anajua Victor Osimhen ni nani, niamini, kila mtu yuko tayari kucheza dhidi yake. Natumai yuko tayari kwa safari iliyo mbele yake."

Uhamishwa wa mkopo kwenda Charleroi ya Ubelgiji ulimfungulia Osimhen milango ya bahati iliyomfanya kuwa bora sana.

Alifunga mabao 20 na kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa timu hiyo. Cha kustaajabisha, Charleroi alianzisha kipengele cha kufanya mkataba huo kuwa wa kudumu Mei 2019 kwa €3.5m pekee, katika hatua iliyowafanya Wabelgiji hao kuuza mali yao mpya kwa Lille ya Ufaransa kwa €12.5m miezi miwili tu baadaye.

"Alikuwa mchezaji mwenye haya sana, mnyenyekevu. Hakuwa mtu wa mazungumzo,'' alisema beki Mfaransa Dorian Dervite ambaye alicheza na Osimhen huko Charleroi.

"Alikuwa na umri wa miaka 18 au 19 - mdogo sana. Lakini alijizatiti kufikia ndoto yake ya kuwa mmoja wa washambuliaji bora wa soka duniani.

"Unaweza kusema kuwa alijitolea sana. Victor amekuwa akifanya kazi kwa bidii sana. Ameimarika sana na anastahili kuwa mahali alipo sasa."

Mabao 18 aliyofunga akiwa Lille yaliifanya Napoli kubisha hodi na hatimaye kuondoka naye.

"Katika soka, ni vigumu kufika kileleni na ni vigumu zaidi kusalia kileleni," alikariri Akpoborie, akitafakari kuhusu uhamisho wa Osimhen kwenda Italia.

"Ndio maana unapaswa kuweka bidii. Kila mtu anatarajia ufunge mabao katika michezo yote unayocheza. Hatua hiyo ya ziada, mbio za ziada, lazima uwe nayo."

Je, Ligi ya Premia ndio 'lengo la mwisho'?

Mapema msimu huu, Osimhen alithibitisha kwamba kucheza Ligi ya Premia ni "ndoto" yake.

Jay Jay Okocha, ambaye alicheza misimu mitano katika ligi kuu ya Uingereza katika vilabu vya Bolton Wanderers na Hull City, anaunga mkono hii inapaswa kuwa matarajio ya mwisho ya mtani wake.

"Ni ligi ambayo inaboresha wachezaji, lazima tu utafute klabu inayofaa ambayo inaendana na mchezo wako," gwiji huyo wa Super Eagles aliambia BBC Michezo Afrika.

"Timu kama Man City, lakini wana (Erling) Haaland sasa. Nafikiri Man United pia inaweza kuwa bora kwake kwa sasa kwa sababu wamekuwa wakihangaika bila mshambuliaji bora katika miaka ya hivi karibuni. Arsenal pia."

Linapokuja suala la kulinganisha na majina makubwa kama Haaland, Dervite hawaamini kabisa uwezo wa Osimhen.

"Takwimu hazidanganyi. Kwangu mimi, Osimhen yuko kwenye kiwango sawa na (Kylian) Mbappe, Haaland na Harry Kane. Kulingana na mimi, amepuuzwa kidogo."