Je spishi za wanyama waliyotoweka zinaweza kurejeshwa?

NASA

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kampuni moja ya Marekani inatarajia kufufua chui wa Tasmanian (kushoto) na tembo wa kale (Woolly Mammoth)n aliyetoweka.

Wanasayansi wanajaribu kufufua aina fulani za wanyama waliotoweka.

Kampuni moja ya Marekani iliyoanzishwa mwaka 2021inasema kuwa inauhakika kwamba inaweza kufufua sio mmoja tu, lakini spishi mbili za wanyama zilizotoweka katika miaka mitano hadi 10 ijayo.

Inaweza kuonekana kuwa ni rahisi katika sinema maarufu ya kutunga ya kisayansi ya Jurassic Park, lakini kwa kweli haionekani kuwa kazi rahisi, na wengi wana shaka juu ya uwezekano wake, pamoja na wale wanaoamini kuwa haifai kuendelea kwa sababu za kimaadili. Katika makala hii tunaangalia mpango huu ni nini, na kuchunguza ikiwa kweli inawezekana kufufua wanyama waliopotea

Mpango ni nini?

Colossal Biosciences, inayoongozwa na mtaalamu wa vinasaba wa Marekani George Church na Mkurugenzi Mtendaji Ben Lamm, inaimani kuwa na uwezo wa kuwafufua tembo wa kale wenye mayoya ifikapo 2027.

Kwa usaidizi wa Chuo Kikuu cha Melbourne, kampuni hiyo hivi karibuni ilitangaza mradi wa kufufua chui jike wa Tasmania, carnivorous marsupial wenye asili katika bara la Australia, Tasmania na New Guinea na waliotoweka tangu miaka ya 1930.

Lakini wanawezaje kufanya hivyo?

NASA

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tembo wa Asia ana DNA sawa na Tembo wa kale

Kuchukua seli shina kutoka kwa viumbe hai na DNA zinazoendana, kisha kutumia teknolojia ya kuhariri jeni "kuunda upya" viumbe vilivyotoweka.

Kwa mamalia wenye manyoya tembo wa kale, mnyama wa karibu zaidi kwa sasa ni tembo wa Asia.

Kuhusu DNA ya chui wa Tasmania, timu hiyo inafanya kazi ya kuchukua seli kutoka kwa kijusi cha chui wa Tasmania ambaye alitolewa kwenye tumbo la uzazi la mama yake na kuwekwa kwenye pombe katika jumba la makumbusho katika jiji la Melbourne nchini Australia.

Kwa nini mchakato wa kumfufua mnyama aliyetoweka ni mgumu?

NASA

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Chui wa Tasmania ametoweka tangu miaka ya 1930

Kikwazo kikubwa kwa wanasayansi ni kupata DNA ikiwa haijakamilika vya kutosha kuweza kumuumba upya kwa usahihi mnyama huyo iliyo karibu iwezekanavyo na DNA ya mnyama wa awali.

Lakini shida ni kwamba wanyama wanapokufa, msimbo wa DNA huvunjika au kugawanywa katika minyororo mifupi, kwa hivyo kuwarudisha pamoja kwa mpangilio unaofaa ni changamoto kubwa.

Je, kuna faida gani?

NASA

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Tasmania devil aliye hatarini anaweza kufaidika na baadhi ya utafiti na teknolojia ya hivi punde
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Ben Lamm, mmoja wa waanzilishi wa Colossal Bioscience, anaamini kwamba kurudisha uhai kwa wanyama waliotoweka kunaweza kusaidia kuhifadhi viumbe hai na kurejesha mifumo ya ikolojia inayopungua na kumaliza uharibifu uliosababishwa na wanadamu hapo awali.

Mamalia wenye manyoya na chui wa Tasmanian walichukua nafasi kubwa katika mazingira yao," anasema. "Kurejeshwa kwa spishi hizi mbili za wanyama kungeathiri vyema mfumo wa ikolojia unaoharibika, unaosababishwa na utupu wa kiikolojia unaosababishwa na kutokuwepo kwa spishi fulani."

Pia anasema kuwa utafiti wa kampuni yao unaweza kuendeleza juhudi za kisayansi zinazolenga kuzuia kutoweka kwa viumbe vingine.

Anaeleza, "Mnyama jike anayejulikana kwa jina la Tasmanian devil au Tasmanian goblin huzaa watoto 20 au 30. Licha ya hayo, ni wachache tu wanao nusuruka kufa. Mbinu tunayotayarisha kwa ajili ya Mradi wa chui wa Tiger inaweza kuwa muhimu sana kwa wahifadhi. ." wanamazingira ambao wanafanya kazi ya kuzuia Tasmania wasiangamizwe.

Ni hatari gani zinazoweza kutokea?

NASA

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini wakosoaji kama vile Victoria Heridge, mwanabiolojia wa mageuzi katika Jumba la Makumbusho la Historia ya Asili huko London, wanabisha kwamba mchakato wa kuunda mtoto wa tembo wa kale unaweza kusababisha hatari kwa wanyama wengine ikiwa kiinitete kilichobadilishwa kinasaba kitapandikizwa ndani ya tembo mbadala

Anaeleza: "Mimba lazima idumu kwa muda wa miezi 22 na kisha mchakato wa kuzaliwa, ambayo ina maana kwamba kuna hatari kwa mama, kubeba aina tofauti kutoka kwake na ni utaratibu wa kuingilia tu."

"Mchakato huu hauwezi kufanyika bila kuwepo kwa tabia zisizo za kimaadaili, ambayo ni matumizi ya matumbo ya mama tembo, ambayo inaweza kuwa ya kutisha. Pia haiwezekani kutumia matumbo ya bandia," anasema.

Lakini Ben Lam anasema Colossal Bioscience inafahamu suala hilo: "Mbali na timu inayohusika na mfumo wa mfuko wa uzazi wa nje, pia tumeunda timu ambayo ina utaalam katika mchakato wa kupandikiza viinitete katika matumbo ya uzazi."

Je, ni mchakato wa kimaadili?

NASA

Chanzo cha picha, Getty Images

Wakosoaji wengine wanaona wazo la kuwarudisha wanyama waliotoweka kama si maadili. Hakuna anayejua kutambulishwa tena kwa spishi kama vile temno wa kale mwenye manyoya, ambaye hajazunguka duniani kwa zaidi ya miaka 4,000. Pia kuna swali la dharura, ambalo ni: Je, wanasayansi wataacha nini ikiwa mafanikio ya teknolojia hii yatathibitishwa?

Victoria anasema ni muhimu kutambua kwamba mnyama yeyote aliyepona kwa njia hii hatakuwa mfano halisi wa mnyama wa asili aliyetoweka.

“Hakuna kitu cha kuwarudisha wanyama waliotoweka, kitakachotokea ni kuundwa kwa kitu kipya kabisa, kitu kikishatoweka maana yake kimetoweka, tumekipoteza na hatuwezi kupata nakala yake halisi."

Lakini Ben Lam anasema kuna hitaji la dharura la kurekebisha makosa ya ubinadamu: "Tuna rasilimali za kufanya kuwarudisha wanyama waliotoweka maishani kuwa ukweli unaoonekana na kuanza kufuta uharibifu ambao binadamu umefanya kwa mifumo ya ikolojia."

Kwa pesa na utaalam wa kisayansi wa mradi huu wa hivi karibuni, tunaweza kuwa karibu kushuhudia ufufuo wa viumbe vilivyotoweka.