Hizi ndio Sababu 7 za kwanini Marekani ilishindwa vita ya Vietnam

Vietman

Chanzo cha picha, Getty Images

Baada ya Vita vya pili vya dunia, Marekani ikawa nchi yenye uwezo mkubwa wa kiuchumi ulimwenguni, na nchi hiyo iliamini kwamba jeshi lake pia lilikuwa na nguvu zote. Lakini baada ya kutumia pesa nyingi na nguvu kazi katika Vita vya Vietnam kwa miaka minane tu, Marekani ilishindwa na vikosi vya Vietnam Kaskazini na washirika wao wa msituni, Viet Cong.

Katika kuadhimisha miaka 50 ya kuwaondoa wanajeshi wa mwisho Marekani kutoka Vietnam (Machi 29, 1973), BBC iliwauliza wataalam wawili na wasomi kujua ni kwa nini Marekani ilipigwa na kushindwa katika vita hivy.

Vita baridi ilikuwa katika kilele chake. Mamlaka za ulimwengu za Kikomunisti na za kibepari baadae zilikabiliana.

Ikifilisiwa na Vita vya pili vya dunia, Ufaransa ilijaribu bila mafanikio kuhifadhi makoloni yake huko Indochina. Katika mkutano wa amani, waligawanya Vietnam ya leo kuwa kaskazini ya kikomunisti na jimbo linaloungwa mkono na Kusini inayoungwa mkono na Marekani.

Lakini kushindwa kwa Wafaransa hakukumaliza mzozo katika nchi hiyo. Waliogopa kwamba ikiwa Vietnam itakuwa ya kikomunisti kabisa, ukomunisti ungeenea hadi nchi jirani. Na hilo ndilo lililoiingiza Marekani kwenye mzozo huo uliodumu kwa muongo mmoja na kugharimu maisha ya mamilioni ya watu.

Kwa hiyo jeshi lenye nguvu zaidi ulimwenguni lilishindwaje katika vita na waasi wataifa jipya lililoanzishwa katika Asia ya Kusini-mashariki?

Wataalamu wawili wana haya ya kusema:

Majukumu ya kivita yalikuwa makubwa sana

Kwenda upande wa pili wa dunia kupigana vita ilikuwa jukumu kubwa. Katika kilele cha vita, kulikuwa na zaidi ya wanajeshi 500,000 wa Marekani waliokuwa kwenye ardhi ya Vietnam.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Gharama ya vita hivi ni ya kustaajabisha. Ripoti ya mwaka 2008 kwa Bunge la Marekani ilisema gharama ya jumla ya vita ilikuwa dola bilioni 68.6 (zaidi ya dola bilioni 95 katika viwango vya leo vya fedha).

Lakini Marekani ilitumia zaidi ya mara nne ya kiasi hicho katika Vita vya pili vya dunia na hatimaye ikashinda. Pia walianzisha vita vya muda mrefu nchini Korea. Kwa hiyo hapakuwa na wasiwasi wa imani katika vichwa vya viongozi wa Marekani kuhusu matokeo ya Vita vya Vietnam.

kutoka Chuo Kikuu cha Uingereza cha St. Andrews, mtaalamu wa sera za kigeni na ulinzi za Marekani, Luke Midap anasema kwamba awali katika vita hiyo kulikuwa na matumaini ya jumla.

"Lilikuwa jambo la ajabu sana kuhusu Vita vya Vietnam," aliiambia BBC, "kwamba Marekani ilikuwa na ufahamu kamili wa matatizo mengi, kulikuwa na shaka nyingi kuhusu kama majeshi ya Marekani yangeweza kuingia katika mazingira hayo. Lakini bado hadi 1968 serikali ya Marekani ilikuwa na uhakika kwamba wao hatimaye watashinda vita."

Lakini imani hiyo ilianza kulegalega, hasa baada ya mashambulio ya Kikomunisti ya Tet mnamo Januari 1968. Hatimaye, Marekani ililazimika kuondoa wanajeshi wake kutoka Vietnam mwaka 1973 huku Bunge la Marekani likianza kupunguza kufadhili vita.

Kama Jeshi la Marekani lilipaswa kuingia Vietnam Dk Midap inaibua maswahilii. Mtaalamu wa pili, Profesa Tung Vu, mkuu wa Idara ya Sayansi ya Siasa katika Chuo Kikuu cha Oregon nchini Marekani, anakubaliana na hilo.

Vikosi vya Marekani havikuwa na vifaa vya kutosha kupigana vita hivyo

Mara nyingi huonekana katika filamu za Hollywood, askari wachanga wa Marekani wanavyopata shida kukabiliana na mazingira magumu ya misitu ya Vietnam. Kwa upande mwingine, waasi wa Viet Cong wakizunguka huku na kule kwenye misitu hiyo isiyo na maji na kufanya mashambulizi ya siri.

Vietman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Zaidi ya wanajeshi 500,000 la wamerakni walipelekwa Vietnam

"Ni vigumu sana kwa jeshi lolote kubwa kufanya kazi katika aina ya mazingira ambayo majeshi ya Marekani yalilazimishwa kupigana," anasema Dk Midap.

"Maeneo mengi yalikuwa na baadhi ya misitu minene zaidi Kusini-mashariki mwa Asia."

Jambo lingine muhimu, kulingana na Midap, ni kwamba waasi waliamua lini na wapi mapigano yangefanyika. Baada ya mashambulio, wangerejea kwenye maeneo salama kuvuka mpaka wa Laos na Cambodia. Vikosi vya Marekani vilipigwa marufuku kuingia katika nchi hizo mbili.

Kulingana na Profesa Vu, lengo la waasi wa Viet Cong lilikuwa ni kuviweka tu vikosi vya Marekani katika nafasi ya kushindwa.

"Waasi wa Vietnam Kusini hawangeweza kamwe kuihodhi Saigon peke yao," aliiambia BBC. Ilikuwa ni hatua mbaya ya kimkakati. Hii iliruhusu wanajeshi wa kawaida wa Jeshi la Kivietinamu Kaskazini kupenya ndani ya Vietnam Kusini, na ni wavamizi hawa ambao hatimaye walishinda vita.

Upinzani wa nyumbani

Vietman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Msitu wa Vietnam ulikuwa hatari na kuleta ugumu kwa pande zote mbili zilizokuwa zinapambana

Kwa mujibu wa kumbukumbu za taifa la Marekani, kufikia mwaka wa 1968, 93% ya nyumba za Marekani zilikuwa na angalau seti moja ya televisheni, na picha za video walizotazama kila siku kwenye TV hizo hazikudhibitiwa zaidi kama ilivyokuwa vita vya awali na zilionyeshwa kwa wakati halisi.

Habari za Vita vya Vietnam tangu 1968 zimejikita zaidi kwenye picha za mauaji, ulemavu na mateso ya raia wasio na hatia. Habari hizi zilikuwa zikiangaziwa kwenye TV na magazeti. Hii iliwatia hofu Wamarekani wengi na mitazamo yao ikageuka kuwa ya kupinga vita.

Maandamano makubwa yalianza kufanyika kote nchini humo.

Vietman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Maandamano ya kupinga vita vya Vietnam yalifanyika huko Marekani

Mnamo Mei 4, 1970, waandamanaji wa amani wanne walipigwa risasi na Walinzi wa Kitaifa katika Chuo Kikuu cha Jimbo la Kent huko Ohio.

"Mauaji ya Jimbo la Kent" yalilikoleza upinzani zaidi wa watu dhidi ya vita.

Inaelezwa takriban wanajeshi 58,000 wa Marekani waliuawa au kutoweka wakiwa vitani Vietnam.

Kulingana na Profesa Vu, hii ilikuwa faida kubwa kwa Vietnam Kaskazini: ingawa pia walipata hasara kubwa, walikuwa na udhibiti kamili juu ya vyombo vya habari vya serikali na ukiritimba wa utoaji wa habari.

"[Vietnam Kaskazini] ilikuwa na mfumo mkubwa wa propaganda. Walifunga mipaka na kuzuia upinzani wowote. Yeyote ambaye hakukubaliana na serikali kuhusu vita alipelekwa gerezani moja kwa moja."

Marekani pia ilishindwa vita vya kushinda mioyo ya Vietnam Kusini

Vita vya Vietnam vilikuwa vita vya kikatili sana. Marekani ilitumia aina mbalimbali za silaha za kutisha katika vita hivi. Mabomu ya napalm na kemikali tofauti zinazoharibu miti kwenye misitu. Hii inasababisha uharibifu mkubwa wa mazao.

Utumiaji wa silaha hizi mbili ulijenga mtazamo wa chuki dhidi ya Marekani kutoka kwa wakazi wa vijijini wa Vietnam Kusini.

Raia wengi wasio na hatia waliuuawa katika vita. Moja ya matukio mabaya zaidi ya Vita vya Vietnam ilitokea mwaka wa 1968. Mamia ya raia wa Vietnam waliuawa na askari wa Marekani katika Massacre My Lai.

Vifo vya raia vilipunguza uungwaji mkono wa Mrekani kutoka kwa raia.

"Siyo kwamba idadi kubwa ya watu katika Vietnam Kusini walikuwa Wakomunisti safi. Watu wengi walitaka tu kuishi na kuepuka vita kwa njia yoyote ile," alisema Dk Midap.

Profesa Vu pia anakubali kwamba Marekani haijafanikiwa sana katika mapambano yake ya kushinda mioyo ya watu.

"Siku zote ni vigumu kwa jeshi la kigeni kufurahisha umma," alisema.

Ari ya Wakomunisti ilikuwa na nguvu

Dk. Midap anaamini kwamba wale waliochagua kupigana upande wa Kikomunisti kwa ujumla walijitolea zaidi kupata ushindi kuliko wale ambao walikuwa wameandikishwa kupigania Vietnam Kusini.

"Baadhi ya utafiti ulifanyika nchini Marekani kulingana na kuhojiwa kwa idadi kubwa ya wafungwa wa kikomunisti wakati wa vita," anasema.

Vietman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Polisi wakikabiliana na waandamanaji huko Marekani

"Rand Corporation, Shirika la utafiti linaloshirikiana na Idara ya Ulinzi ya Marekani na jeshi la Marekani, lilifanya tafiti hizi juu ya motisha na ari ya wafungwa. Walitaka kujua kwa nini Wavietnam wa Kaskazini na Viet Cong wanapigana vita hivi. Na taasisi mbili zilihitimisha kwa kauli moja kuwa motisha ya wafungwa inatokana na uzalendo. . Yaani walitaka kuunganisha nchi na kuunda serikali moja."

Uwezo wa vikosi vya Kikomunisti kuendelea kupigana licha ya mauaji makubwa ya msituni labda ni ushahidi wa ari yao.

Takriban wapiganaji milioni 1.1 wa Vietnam Kaskazini na Viet Cong waliuawa wakati wa vita. Lakini bado wakomunisti waliweza kujenga jeshi lao hadi dakika ya mwisho ya vita.

Profesa Vu, hata hivyo, hajashawishika kabisa kuwa ari ya Kivietinamu Kaskazini ilikuwa kubwa na yenye nguvu. Lakini anakiri kwamba jinsi wanajeshi wa kaskazini walivyovurugwa akili kulifanya kila askari kuwa silaha.

"Waliweza kuwafanya watu kuamini mawazo yao. Kupitia propaganda na elimu walifanikiwa kuwageuza watu risasi."

Serikali ya Vietnam Kusini haikuwa maarufu na ilitawaliwa na ufisadi

Vietman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wapiganaji wawili wa Viet Cong wakiwa kwenye mikono ya Jehsi la Marekani

Kwa mujibu wa Dk. Midap, tatizo linaloikabili serikali ya Vietnam Kusini ni kutokuwa na imani na uhusiano wake na mataifa yaliyokuwa ya kikoloni.

"Mgawanyiko kati ya Vietnam ya Kaskazini na Kusini daima umekuwa bandia, ulijengwa kutokana na Vita Baridi," anasema, akiongeza kuwa "hakukuwa na sababu za kitamaduni, kikabila au ya kiisimu kugawanya Vietnam kuwa nchi mbili."

"Kuwepo kwa wanajeshi 500,000 wa Marekani chini nchini Vietnam kulionyesha ukweli kwamba serikali hii ilikuwa tegemezi kwa wageni kwa kila njia," Dk. Midap anasema.

"Vietnam Kusini haikuweza kujenga mtizamo ambao ungewashawishi raia kwamba mapambano yalikuwa mapambano ya maisha na kifo."

Hili, anasema, linazua swali la iwapo hata ilikuwa muhimu kutuma wanajeshi wa Marekani katika nchi iliyojaa ufisadi.

"Tangu kuanzishwa kwake hadi kufa kwake [Jamhuri ya Vietnam] ilikuwa nchi yenye ufisadi sana," anasema, akiongeza kuwa "msaada mkubwa wa Marekani kutoka miaka ya 1960 hadi 1975 ulifanya ufisadi wa nchi kuwa mbaya zaidi. Ufisadi uliokithiri ulidumaza kabisa uchumi wa Vietnam Kusini."

"Wakati huo hakuna mtu ambaye angeweza kushikilia wadhifa wa kiraia au kijeshi bila kutoa hongo." Alihisi ilikuwa na athari kubwa kwa vikosi vya jeshi.

"Hii ilimaanisha kuwa Marekani haiwezi kamwe kujenga jeshi la kuaminika na lenye ufanisi la Vietnam Kusini," anasema.

"Kwa hiyo ilikuwa ni jambo lisiloepukika - na Rais Richard Nixon alitambua - kwamba wakati fulani katika siku zijazo wakati askari wa Marekani watakapoondoka na kurudi nyumbani, Vietnam Kusini ingeanguka mara moja."

Baadhi ya mapungufu, ambayo Vietnam ya Kaskazini haikuwa nayo

Vietman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Wavietnam walikuwa na ari kubwa ya kupigana kuliko wapinzani wao

Lakini Profesa Vu hakubaliani na sababu kwamba ufisadi Vietnam Kusini ilikuwa sababu ya moja kwa moja kwa Mrekani kushindwa. Anadhani kwamba tafiti zilizofuata za Vita vya Vietnam kwa ujumla zimejielekeza kutafuta visingizio.

"Wanataka mtu wa kulaumiwa kwa kushindwa huku, na mahali rahisi pa kulaumiwa ni Wavietnam Kusini," anasema, akiongeza kuwa ripoti za Marekani zimezidisha madai ya rushwa na upendeleo dhidi ya Wakatoliki.

"Rushwa ilikuwa imekithiri, lakini haikuwa katika kiwango kilichosababisha kushindwa vita. Vitengo vingi vya kijeshi visivyo na ufanisi na visivyofaa viliundwa, lakini kwa ujumla jeshi la Vietnam Kusini lilipigana vizuri sana," anasema.

Kati ya wanajeshi 200,000 na 250,000 wa Vietnam Kusini walipoteza maisha wakati wa vita. Profesa Vu anadhani, kwa hiyo, ingekuwa bora kwa Vietnam Kusini kama wangefanya kila wawezalo kushinda vita, hata kwa silaha na ufadhili wa Marekani.

Vietman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Rais Nixon aliamini kuwa kuondoa vikosi vyake kungeidondosha serikali ya Vietnam Kusini

Profesa Vu anasema kwamba hatimaye hatima ya vita iliamuliwa na uwezo wa Vietnam Kaskazini kupambana vita kwa ujumla. Juhudi hizo hazikuonekana Vietnam Kusini.

Asili ya mfumo wa kisiasa huko Vietnam Kaskazini ilimaanisha kuwa umma uliamini katika vita na walijua kidogo kuhusu majeruhi.

Vietman

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Vikosi vya Vietnam vilikuwa vinauwezo wa kujitolea kufanya mashambulizi ya kujitoa mhanga, wanasonga tu kwa adui bila kuogopa na kwa wingi wao, kitu ambacho Marekani haikuweza kufanya

"Wakomunisti waliweza kujenga mtazamo wa umma kwa njia ambayo Marekani na Vietnam Kusini hazingeweza," alisema Profesa Vu.

"Waliweza kukusanya askari licha ya kupoteza watu wengi," alibainisha, akimaanisha kwamba Vietnam Kaskazini inaweza kutumia mbinu za kijeshi kama vile mashambulizi ya kujiua ambayo Vietnam Kusini haikuweza."

Kilichokuwa muhimu zaidi, aliongeza, ni kwamba licha ya uungaji mkono wa Marekani kwa Vietnam Kusini, hakukuwa na harakati za usaidizi wa kifedha na kijeshi kutoka Umoja wa Kisovieti na Uchina kwenda Vietnam Kaskazini.