Haaland, Bellingham, Vinicius, Mbappe: Nani atashinda taji la Ballon d'Or 2024?

Chanzo cha picha, Getty Images
Mabadiliko ya walinzi yanakaribia kufanyika kwenye kilele cha soka la wanaume.
Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambao wameshikilia taji la Ballon d'Or kwa muda mrefu zaidi katika miaka 15 iliyopita, wanatazamiwa kucheza nchini Saudi Arabia na Marekani mtawalia msimu ujao.
Karim Benzema, mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia mwaka 2022, amefuata nyayo za Ronaldo kwa kuhamia Saudi Arabia, wakati mshindi mwingine pekee katika kipindi hicho - Luka Modric mwenye umri wa miaka 37 - anafikia mwisho wa safari yake kitaaluma licha ya kunasemekana kuwa atakubali kusalia Real Madrid msimu ujao.
Messi anatarajiwa kushinda tuzo ya Ballon d'Or ya 2023 baada ya kuiongoza Argentina kutwaa taji la kwanza la Kombe la Dunia tangu 1986 msimu wa baridi uliopita, lakini ni nani atakayevaa taji hilo 2024?
BBC Sport inaangazia hilo…
Jude Bellingham (Real Madrid)
Mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri kwenye Kombe la Dunia mwaka jana nchini Qatar, Bellingham alikua kijana wa tatu kuuzwa kwa bei ghali zaidi katika historia - na mchezaji wa pili wa Uingereza ghali zaidi wakati wote - alipojiunga na Real Madrid kwa euro 103m za awali (£88.5).
Hakuweza kuiongoza klabu hiyo ya Bundesliga kutwaa taji la kwanza la ligi baada ya miaka 11 lakini akafanya vyema katika msimu wake wa mwisho nchini Ujerumani, akiweka historia Oktoba mwaka jana alipofanywa nahodha mwenye umri mdogo zaidi katika klabu hiyo akiwa na umri wa miaka 19 pekee.
Bellingham, ambaye aliondoka Birmingham City na kwenda Dortmund kwa £25m mwaka 2020, alisajili mabao 14 na pasi saba zilizosaidia katika mechi 42 msimu wa 2022-23.
Baada ya kukataa vilabu vingi vya Uropa na kuwapendelea mabingwa hao mara 14 wa Uropa, kiungo huyo wa kati anatazamia kudumisha taaluma yake katika mji mkuu wa Uhispania.
Erling Haaland (Manchester City)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mchezaji wa kwanza kushinda tuzo za mchezaji bora wa Ligi ya Premia na mchezaji chipukizi wa mwaka katika msimu huo huo, raia huyo wa Norway pengine hata ndiye mrithi dhahiri zaidi wa Ronaldo, Messi na wenzake.
Haaland ameweka rekodi katika kampeni yake ya kwanza kujitokeza kwenye ligi kuu ya England, mabao yake 36 yakivunja rekodi bora iliyowekwa na Alan Shearer na Andy Cole (34) kwa karibu miongo mitatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 alimaliza msimu akiwa na mabao 52 katika mechi 53, na kumfanya kuwa mchezaji wa pili pekee katika historia ya ligi kuu ya Uingereza - na wa kwanza katika miaka 95 - kufunga zaidi ya mara 50 katika mashindano yote.
Tayari akiwa na mabao 229 katika maisha ya soka kwa klabu na taifa, anaweza kuvunja rekodi ya muda wote ya Ronaldo ya 837.
Vinicius Jr (Real Madrid)
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Baada ya Madrid kuifunga Liverpool katika hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa mwezi Machi, kocha mkuu Carlo Ancelotti alimtaja Vinicius "mchezaji madhubuti zaidi popote duniani - anayeamua mechi nyingi kwa msingi thabiti".
Mbrazil huyo, ambaye aliiogopesha safu ya ulinzi ya Manchester City kwa kasi na ujanja wake katika nusu fainali ya 2021-22 kabla ya kufunga bao la ushindi kwenye fainali dhidi ya Liverpool, alikuwa na mabao 23 na amesaidia mara 21 kufunga magoli katika michuano yote 22-23 - akiwa wa tatu kwa wingi wa mabao katika Ligi za daraja la juu barani Ulaya nyuma ya Haaland na Kylian Mbappe.
Mlengwa wa unyanyasaji wa ubaguzi wa rangi mara nyingi msimu uliopita, tukio moja mahususi lililomhusisha Vinicius huko Valencia lilizua hasira nchini Uhispania na Brazili.
Watu saba baadaye waliadhibiwa kwa vitendo vya ubaguzi wa rangi, Valencia waliadhibiwa kwa kufungiwa sehemu ya uwanja na Vinicius mwenyewe aliajiriwa na Fifa kuwa sehemu ya kikosi kazi kipya cha kupinga ubaguzi wa rangi.
Kylian Mbappe (Paris St-Germain)

Chanzo cha picha, Getty Images
Mfaransa huyo mahiri amefunga mabao 212 na kusaidia mara 98 katika michezo 260 tangu ajiunge na Paris St-Germain kutoka Monaco mwaka 2017, na kuchangia mataji 13 ya ndani akiwa na klabu hiyo inayomilikiwa na Qatar.
Akiwa sehemu muhimu ya Ushindi wa Kombe la Dunia la Ufaransa mwaka 2018, Mbappe pia amesajili mabao 38 katika mechi 88 akiwa na Les Blues, na kumfanya kuwa nafasi ya tano katika orodha ya wafungaji bora wa muda wote - na mabao 15 tu nyuma ya Olivier Giroud anayeshikilia rekodi kwa sasa.
Alinyimwa ushindi wa mfululizo wa Kombe la Dunia na Argentina iliyoongozwa na Messi, licha ya kufunga hat-trick ya kwanza na ya mwisho tangu Geoff Hurst wa Uingereza mwaka 1966.
Baada ya kuiarifu PSG kwamba hataongeza mkataba wake zaidi ya 2024, hakutakuwa na upungufu wa mashabiki zake ikiwa mabingwa hao wa Ufaransa wataamua kumnunua mshambuliaji huyo msimu huu wa joto.
Neymar (Paris St-Germain)

Chanzo cha picha, Getty Images
Akiwa na umri wa miaka 31, Neymar sio mgeni kwenye mchezo lakini hadhi ya Mbrazil huyo kama mmoja wa nyota wakubwa wa mchezo bado haijabainishwa.
Winga huyo alisajili mabao 35 katika michuano yote msimu uliopita, licha ya kukosa miezi mitatu ya mwisho ya kampeni kutokana na majeraha ya kifundo cha mguu.
Novemba mwaka jana, Neymar aliifikia rekodi ya Pele ya kufunga mabao 77 kwa bao lake la robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Croatia.
Ni suala la muda tu kabla ya rekodi hiyo kuwa yake.















