Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Aston Villa sasa yavutiwa na Nicolas Jackson wa Chelsea

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mshambuliaji wa Chselsea Nicholas Jackson
Muda wa kusoma: Dakika 3

Aston Villa inachunguza uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa Senegal Nicolas Jackson, 24, kutoka Chelsea lakini bei inayotakiwa inapaswa kuwa chini ya £60m kutokana na vikwazo vya kifedha vya klabu hiyo ya West Midlands. (Telegraph - Subscription)

Uhamisho wa Bayern Munich kumnunua fowadi Mfaransa Christopher Nkunku, 27, umekwama, na hivyo kuchelewesha majaribio ya Chelsea kumsajili kiungo wa kati wa RB Leipzig na Uholanzi Xavi Simons, 22. (Guardian)

Chelsea wanatazamia kuongeza juhudi zao za kumsajili fowadi wa Argentina Alejandro Garnacho kutoka Manchester United lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 hataruhusiwa kuondoka Old Trafford kwa bei nafuu. (Evening Standard)

Newcastle haiko tayari kulipa zaidi ya pauni milioni 40 kumnunua mshambuliaji wa Brentford Yoane Wissa lakini The Bees wameweka bei ya pauni milioni 60 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa DR Congo mwenye umri wa miaka 28. (Northern Echo )

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Yoane Wissa

Mshambulizi wa Wolves Jorgen Strand Larsen bado anavutiwa na Newcastle - ingawa Mnorwey huyo mwenye umri wa miaka 25 hana mpango wa kuondoka Molineux. (The Athletic - Subscription)

Tottenham wamemlenga kiungo mshambuliaji wa Monaco mwenye thamani ya pauni milioni 47.5 Maghnes Akliouche, 23, kama mbadala wa bei nafuu kwa winga wa Brazil Savinho huku Manchester City wakidai pauni milioni 70 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21. (Independent)

Crystal Palace inamtaka winga wa Southampton, Tyler Dibling, 19, kuchukua nafasi ya Mwingereza mwenzake Eberechi Eze, 27, ambaye uhamisho wake wa kwenda Tottenham unakaribia. (Sportsport)

Kiungo wa kati wa Brazil Douglas Luiz, 27, anatazamiwa kujiunga na Nottingham Forest kutoka Juventus baada ya mmiliki wa Forest Evangelos Marinakis kufanya makubaliano na meneja mkuu wa klabu hiyo ya Turin Damien Comolli. (Tuttosport - Itali),

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Okafor

Leeds wako tayari kumsajili mshambuliaji wa Uswizi Noah Okafor, 25, kutoka AC Milan kwa mkataba wa thamani ya £18.4m (euro 21m). (Sky Sports Italia - In Itali),

Wolves na West Ham wote wanavutiwa na kiungo wa kati wa Uhispania Marc Casado lakini wanakabiliwa na swali gumu la kumshawishi mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 kuondoka Barcelona. (Marca - In Spanish),

West Ham wanakaribia kukamilisha mkataba ambao utamruhusu kiungo wa kati wa Mexico Edson Alvarez, 27, kujiunga na Fenerbahce kwa mkopo. (Sportsport)

Espanyol wako kwenye mazungumzo na Burnley juu ya kumsajili tena mshambuliaji wa Italy U21 mwenye umri wa miaka 20 Luca Koleosho kwa mkopo wa msimu mzima. (Sky Sports)

Uhamisho wa fowadi wa Brazil Rodrigo Muniz kutoka Fulham kwenda Atalanta umezimwa baada ya Cottagers kukataa mpango uliopendekezwa wa pauni milioni 35 kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 kutoka klabu hiyo ya Serie A. (Fabrizio Romano)