Je, ni nini kilichotokea kwa Mbappe na Ufaransa?

.

Chanzo cha picha, PA Media

Maelezo ya picha, Kylian Mbappe

Hakuna mchezaji aliyekosa nafasi nyingi kama Kylian Mbappe kwenye Euro 2024 akiwa na fursa 24 na bao moja pekee la penalti.

Baada yake ni Cristiano Ronaldo, ambaye hangeweza kutumia nafasi zake 23 na kufunga bao.

"Ndoto yangu ilikuwa kushinda ubingwa wa Uropa, lakini matokeo ya kazi yetu yalikuwa kufeli."

Hii ilikuwa tathmini ya wazi ya Kylian Mbappe, bingwa wa Kombe la Dunia, ambaye alitarajiwa kuwa na uwezo wa kuiongoza Ufaransa kutwaa ubingwa huko Ujerumani.

Mchezaji huyo mwenye thamani ya pauni milioni 190, ambaye hatimaye alitimiza ndoto yake ya kuhamia Real Madrid mwaka huu, alicheza vyema kama nahodha wa Ufaransa katika michuano ya Euro 2024.

Lakini Mbappe, ambaye miaka miwili iliyopita aliweza kufunga hat-trick katika fainali za Kombe la Dunia na kufikia rekodi ya Sir Geoff Hurst (nyota wa soka la Uingereza miaka ya zamani), hakuweza kuwa na ufanisi mkubwa, na Wafaransa hao walioonekana wazembe.

Timu hiyo iliondolewa katika mashindano hayo kwa kushindwa katika nusu fainali mjini Munich dhidi ya Uhispania.

‘Mchawi’ wa Kombe la Dunia, nini kilichotokea Euro?

Mbappe alipata umaarufu akiwa kijana kwenye Kombe la Dunia la 2018 nchini Urusi, akiifungia Ufaransa mara nne waliposhinda tena Kombe la Dunia baada ya miaka ishirini.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kisha alifunga mabao manane ya ajabu kwenye Kombe la Dunia la 2022, ikiwa ni pamoja na hat-trick kwenye fainali dhidi ya Argentina. Mechi iliyoisha baada ya Ufaransa kushindwa kupitia mikwaju ya penalti na Argentina.

Kushiriki katika makombe mawili ya Dunia na mafanikio katika kufunga mabao kumi na mbili kulimfikisha kwenye rekodi ya mabao yaliyofungwa na Pele, gwiji wa Brazil katika Kombe la Dunia.

Lakini Mbappe hakufanikiwa katika Euro 2020 na hakuweza kufunga bao. Kukosa penalti yake katika mikwaju ya penalti kulisababisha Ufaransa kuondolewa katika hatua ya 16 bora dhidi ya Uswizi.

Katika Euro 2024, alikwenda Ujerumani akiwa na matumaini makubwa, akapigana tena na kufunga penalti katika sare ya 1-1 kwenye mechi ya hatua ya makundi dhidi ya Poland.

Lakini matokeo haya yaliifanya Ufaransa kuondolewa kileleni mwa jedwali na kukabiliwa na droo ngumu zaidi katika hatua ya mchujo.

Mbappe alishambulia mara 9 kwenye lango wakati wa mchuano huo. Lakini angeweza kutengeneza nafasi tatu pekee, ikiwa ni pamoja na pasi yake nzuri ya bao la kwanza la Randall Kolo-Moani dhidi ya Uhispania.

.Beki wa zamani wa Uingereza Rio Ferdinand aliiambia BBC: "Mbappe alipiga pasi nzuri, lakini huo ulikuwa wakati pekee wa ubora ambao Ufaransa walionyesha."

"Kiasi hiki hakitoshi kwa mchezo uliokuwa na umuhimu wa kiasi hiki. Mbappe hakika atasikitishwa na uchezaji wake katika mashindano haya. Kwa sababu hii haikuwa kile tulichotarajia kutoka kwake."

Katika mechi kumi na nne za Kombe la Dunia, Mbappe ana wastani wa mabao 1.11 na asisti kwa dakika 90. Wakati kiwango hiki ni 0.32 tu katika michezo yake 9 katika mashindano ya Euro.

Nafasi yake muhimu zaidi katika nusu fainali ilikuja mwishoni mwa mechi, ambapo alipenya safu ya ulinzi ya Uhispania lakini akapiga shuti lake hewani.

Mtaalamu wa soka wa Ufaransa Julien Laurent aliiambia BBC: "Amefunga mara elfu moja katika maisha yake ya soka katika matukio kama haya.

"Mbappé hakutumia nafasi yake na katika nyakati muhimu zaidi, Ufaransa haikunufaika na ‘uchawi’ wake.

."

Kila kitu kilikataa

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kylian Mbappe

Bila shaka, Mbappe aliathiriwa na pua yake iliyovunjika katika dakika za mwisho za mechi ya kwanza ya Ufaransa dhidi ya Austria. Jeraha hili lilimfanya akose mchezo dhidi ya Uholanzi, na katika mchezo dhidi ya Poland, ambapo aliweza kufunga, alionekana uwanjani na barakoa.

Kuvaa barakoa kulisababisha matatizo kwa Mbappe na nilimwona akisogeza kifaa hicho mara kwa mara wakati wa mechi, hadi mwishowe akakitoa dhidi ya Uhispania.

Alipoulizwa iwapo jeraha hilo limemzuia, mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alisema kwa urahisi: "Kulikuwa na sababu nyingi.

Usizidishe, nzuri au mbaya, yote yamekwisha. Sikuwa sawa na tunarudi nyumbani.

Kocha mkuu wa Ufaransa, Didier Deschamps, hapo awali alikiri kwamba barakoa ya Mbappé ilimletea matatizo. Lakini baada ya kushindwa dhidi ya Uhispania, alisema: "Kutumia barakoa ilikuwa ni usumbufu kwake na hakuna zaidi." "Sitaki kuweka jukumu la kushindwa kwa mchezaji mmoja."

"Unapofika nusu fainali na ukakutana na timu yenye ubora kama Uhispania, lazima uwe katika ubora wako. Ingawa hatukuwa hivo

Je, hatua inayofuata ya Mbappe itakuwa ipi?

Baada ya kushinda mataji saba ya Ligue 1 akiwa na Monaco na Paris Saint-Germain, anachezea Real Madrid kwa lengo la kushinda Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Ambapo watafanya kombinesheni kubwa ya kushambulia na Jude Billingham, Vinicius Mdogo na Rodrigo.

Amesema ataenda likizo baada ya Euro na kupumzika ili kucheza kwa nguvu na nguvu zaidi katika jiji jipya na na meneja mpya. Kila kitu kinategemea Carlo Ancelotti kuanzia sasa

Imetafsiriwa na kuchapishwa na Seif Abdalla