Ni wakati gani bora wa siku kufanya mazoezi?

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuna ushahidi unaoongezeka kwamba wakati wa siku tunaofanya mazoezi huleta tofauti kwa ufanisi wetu na kimichezo na afya, lakini je, tunaweza kufundisha miili yetu kufikia kilele cha ufanisi wetu kwa nyakati tofauti za siku?

Katika miezi michache, wanariadha wakuu duniani watakusanyika Paris kushindana kuwania tuzo ya mwisho katika michezo – ambayo ni dhahabu katika Michezo ya Olimpiki. Kwa wale wanaotarajia kupata fursa ya kuingia kwenye vitabu vya historia na kuvunja rekodi, wanaweza kutaka kuangalia saa kabla kuwa kwenye viunga vyao vya kuanza mashindano.

Angalau waogeleaji wanaweza, kulingana na utafiti mmoja wa kisayansi. Katika michezo minne ya Olimpiki huko Athens (2004), Beijing (2008), London (2012) na Rio (2016), nyakati za kuogelea za waogeleaji 144 walioshinda medali zilipatikana kuwa za haraka zaidi waliposhindana katika saa za mapema za jiona. Kwa ujumla karibu medali zote zilipatikana saa kumi na moja na dakika 12 jioni. Ni sehemu ya ushahidi unaoongezeka unaoonyesha kuwa utendaji wa kimwili huathiriwa na nyakati za siku.

Matukio haya hayapatikani tu miongoni mwa wanamichezo wenye medali - waendesha baiskeli pia wameonekana kukamilisha malengo yao ya umbali wanaotaka kuendesha baiskeli saa za jioni kuliko muda mwingine.

Michezo ya ushindani huathiriwa sana na muda wa kati ya saa kumi za jioni na saa mbili za usiku. Wakati wa siku pia unaonekana kusababisha utendaji wa wanamichezo wanaume na wanawake tofauti wanapofanya mazoezi.

Lakini vipi ikiwa ratiba yako inamaanisha kuwa una muda wa kufanya mazoezi saa moja asubuhi? Kuna dalili kadhaa inaweza hata kuwa inawezekana kurekebisha wakati wako wa ufanisi kwa utendaji wa riadha.

Mtu anaweza labda kuboresha matokeo mfumo wa mwili wa mazoezi kulingana na wakati wake wa mazoezi – Juleen Zierath

Utofauti katika utendaji wetu kwenye michezo au mazoezi ya mwili hutokana na utendaji wa mwili unaohusika na kudhibiti tabia kama vile usingizi na hamu ya chakula katika kipindi cha saa 24.

Juleen Zierath, mtaalamu wa mazoezi ya mwili katika Taasisi ya Karolinska nchini Sweden, amekuwa akifanya utafiti wa uhusiano kati ya mazoezi na mfumo wa utendaji wa mwili was aa 24 (circadian). Yeye na wenzake walibaini kuwa panya ambao walifanya mazoezi asubuhi waliweza kuchoma mafuta ndani ya miili yao zaidi.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Zierath anasema matokeo yanaonyesha kuwa kufanya mazoezi kwa wakati mzuri wa siku kunaweza kuongeza faida za kiafya zinazotokana na mazoezi kwa watu wenye magonjwa yanayotokana na mfumo wa utendaji wa mwili kama vile kama vile aina ya kisukari inayotokana na mtindo wa maisha.

"Kila mtu anakubali kuwa mazoezi ni muhimu, bila kujali muda wa siku, lakini mtu anaweza kuboresha matokeo ya utandaji wa mwili kwa mazoezi kulingana na wakati unaofanya mazoezi," anasema Zierath.

Matokeo yao yanaonyesha utafiti wa hivi karibuni kwa wanadamu ambao ulionyesha kufanya mazoezi ya mafunzo mashindano, mbio za muda, na ya ustahimilivu kwa saa moja kwa siku asubuhi kwa wiki inaweza kupunguza mafuta ya tumbo na shinikizo la damu kwa wanawake.

La kushangaza ni kwamba wakati wanawake walipofanya mazoezi sawa jioni, utendaji wao wa misuli uliimarika.

Kwa wanaume, mazoezi ya jioni yalisaidia kupunguza shinikizo la damu na kuchochea kupungua kwa mafuta ya mwili.

Lakini utafiti katika eneo hili bado unaendelea na uchambuzi wa hivi karibuni wa tafiti zilizopita unaonyesha kwa kiasi fulani ushahidi usio na maana kwa athari ya faida ya wakati wa siku juu ya ufanisi wa mazoezi au faida za kiafya.

h

Chanzo cha picha, Getty images

Maelezo ya picha, Unaweza kupata ufanisi bora zaidi jioni kuliko asubuhi unapofanya mazoezi kama vile ya kunyanyua uzani

Sababu moja ya hili ni karibu tofauti zilizopo kati ya watu binafsi. Kwa mfano, nyakati za kilele za ufanisi wa riadha hutofautiana.

"Kuna tofauti katika muda wa saa zetu," anasema Karyn Esser, mtaalamu wa mazoezi ya viungo katika Chuo Kikuu cha Florida cha Gainesville nchini Marekani. "Baadhi yetu tunaweza kukimbia kidogo, na wengine wana saa ambayo wanaweza ndani ya saa 24."

Kundi la watafiti wakiongozwa na Esser, waligundua kuwa ustahimilivu thabiti unaoendesha mafunzo kati ya panya asubuhi unaweza

w

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Kuogelea asubuhi inaweza kuwa burudani kwako, lakini una uwezekano mdogo wa kuvunja rekodi yoyote katika mchezo huo

Utafiti wa hivi karibuni, ambao bado haujachapishwa katika jarida uligundua kuwa ukubwa wa mabadiliko katika ufanisi ulikuwa wa hali ya juu kwa panya waliofunzwa kufanya mazoezi ya mwili asubuhi ikilinganishwa na wale waliofunzwa mchana. Baada ya wiki sita za mafunzo, panya wa asubuhi na mchana waliweza kufikia utendaji sawa wa mazoezi ya ustahamilivu.

Watafiti wanapendekeza kwamba ikiwa athari sawa inapatikana kwa wanadamu, inaweza kuwa inawezekana kwa wanariadha kurekebisha "saa zao za ndani ya miili yao " na mafunzo sahihi. Kuna ushahidi wa awali kwamba mazoezi yanaweza kubadilisha utendaji wa miili ya wanadamu, na kuifanya iwe muhimu na kuwa na ufanisi zaidi katika mazoezi hayo.

"Wazo rahisi hapa ni kwamba tunapaswa kuzingatia saa ambazo misuli yetu inafanya kazi yema wakati wa mazoezi ya miili yetu ili kupata kilele cha ufanisi wetu ," anasema Esser.

Mazoea ya viungo ya kila siku yanaonekana kuwa ni muhimu - mwili wetu hubadilishwa na mazoezi wakati yanapofanya mara kwa mara wakati kwa wakati ule ule wa siku kila siku.

"Ikiwa uko katika idadi ya watu, au hata mwanariadha wenye ujuzi huo, na unapanga kushiriki mashindano, unapaswa kujaribu kuwa na mafunzo maalum ya siku ya mbio," anasema Zierath.

Watafiti wengi wana nia ya kuonyesha, hata hivyo, kwamba kufanya mazoezi wakati wowote ni faida.

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Ambia Hirsi