Ufichuzi wa Pentagon waonesha S Korea ina wasiwasi kuhusu kutuma silaha Ukraine

Chanzo cha picha, EPA
Nyaraka za Pentagon zilizovuja zinaonekana kufichua mazungumzo nyeti kati ya maafisa wa ngazi ya juu wa Korea Kusini kuhusu kutuma silaha Ukraine.
Waraka huo wa siri, ulioonekana na BBC, unaonesha kwamba Marekani imekuwa ikimpeleleza mshirika wake wa miongo kadhaa Korea Kusini.
Ilikuwa katika ufichuzi unaojumuisha habari kuhusu vita vya Ukraine, na vile vile kuhusu China na washirika wa Marekani.
Ufichuzi huo unaweza kuvuruga uhusiano wa Korea Kusini na Marekani na Urusi.
Korea Kusini inasema inachunguza uvujaji huo lakini imesisitiza kuwa haiwezekani kuzuia mazungumzo ya faragha ndani ya ofisi yake ya rais, na kwamba mjadala huu haungeweza kufanyika katika chumba chake cha faragha cha chini ya ardhi.
Washington imekuwa ikihangaika kutafuta chanzo cha ufichuzi huo, jambo ambalo Pentagon inasema ni hatari kubwa kwa usalama wa taifa.
Hati iliyoonekana na BBC inaonyesha kuwa Korea Kusini ilichangsnyikiwa kati ya kuuza risasi ambazo zingeweza kutumiwa na Ukraine.
Washington imekuwa ikishinikiza Seoul kuipatia Kyiv silaha, lakini hadi sasa imepinga, ikitoa mfano wa sera yake ya kutosambaza silaha kwa nchi zinazopigana.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Mwaka jana, Korea Kusini ilikubali kuwa itaiuzia Marekani makombora ya mizinga, ili kujaza hifadhi zake ambazo zimepunguzwa na vita vya Ukraine.
Kama sehemu ya mpango huo, Seoul ilisisitiza kwamba Marekani lazima ijihifadhie makombora hayo yenyewe, hayawezi kuelekezwa Kyiv. Ripoti iliyofichuliwa inaonyesha kuwa serikali ilikuwa na wasiwasi juu ya mpango huo na inashuku kuwa Marekani inaweza kusambaza mizinga hiyo kwa Ukraine.
Inafafanua mazungumzo nyeti na ya hali ya juu kuanzia tarehe 1 Machi 2023 kati ya washauri wawili wakuu wa usalama wa Rais wa Korea Kusini Yoon Suk Yeol.
Mshauri wa waziri wa mambo ya nje wa Rais Yoon Yi Mun-hui aliripotiwa kumwambia Mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa wakati huo Kim Sung-han kwamba serikali "imezama katika wasiwasi kwamba Marekani haitakuwa mtumiaji wa mwisho" wa risasi hizo.
Pia walikuwa na wasiwasi kwamba Rais Biden anaweza kumpigia simu Rais Yoon moja kwa moja kuhusu suala hilo, na kwamba ikiwa Korea Kusini ingebadili sera yake ya kutoa silaha kwa Ukraine, inaweza kuonekana kana kwamba imeshinikizwa na Marekani.
Kulingana na waraka huo, mshauri wa usalama wa taifa wa Korea Kusini, Bw Kim, kisha akapendekeza wangeweza kuiuzia Poland makombora badala yake, ikizingatiwa kwamba "kupata risasi hizo kwa Ukraine haraka ndilo lilikuwa lengo kuu la Marekani".

Chanzo cha picha, Getty Images
Marekani haijaficha ukweli kwamba inataka Seoul kuipatia Ukraine silaha. Inaamini kuwa Korea Kusini, pamoja na uwezo wake wa kutengeneza silaha za hali ya juu kwa kasi kubwa, inaweza kutoa mchango mkubwa katika matokeo ya vita hivyo.
Lakini Seoul imekuwa ikisita kufanya hivyo, kwa hofu ya kuharibu uhusiano wake na Urusi. Uvujaji huu unaonyesha kwamba Seoul haikuelewa tu kwamba makombora ya Korea Kusini yanaweza kuishia Ukraine, lakini kwamba walikuwa wazi kwa hili kutokea, suala ambalo linaweza kudhoofisha uhusiano wake na Urusi.
"Korea Kusini kila mara hutekeleza kitendo hiki cha kusawazisha, huku Marekani ikiwa upande mmoja, na Urusi na China kwa upande mwingine," alisema Jenny Town, mchambuzi wa Korea kutoka taasisi ya 38 North. "Uvujaji huu unaonyesha ni mikakati wanayojali zaidi. Wanajaribu kusawazisha kile ambacho wako tayari kufanya ili kuunga mkono Ukraine na jinsi itakavyochukuliwa."
Wakati wa kuvuja ni bahati mbaya. Katika muda wa wiki mbili Rais Yoon atasafiri hadi Ikulu ya White House katika ziara ya kiserikali kusherehekea miaka 70 ya muungano kati ya nchi hizo mbili - muungano ambao Marekani iko katika maumivu kuashiria bado "ni mgumu".
Hili limezusha wasiwasi wa kiusalama mjini Seoul, huku chama cha upinzani kikihoji ni vipi Marekani iliweza kuingilia mazungumzo hayo ya ngazi ya juu. "Huu ni ukiukaji wa wazi wa mamlaka yetu na Marekani na ukiukaji mkubwa wa usalama kwa upande wa Korea Kusini," ilisema katika taarifa siku ya Jumatatu.
Kim Jong-dae, mshauri wa serikali ya zamani ya kiliberali, anaelezea hili kama "janga la kijasusi" kwa Wakorea Kusini. "Hii ni ncha ya barafu. Hakuna njia katika kuzimu ni hii," alisema.
Serikali ya Korea Kusini inajaribu kupuuza uvujaji huo. Inasema inakubaliana na tathmini ya Marekani kwamba huenda baadhi ya nyaraka zimepotosha.
Wakati huo huo chanzo cha serikali kilionya kwamba jaribio lolote la "kutia chumvi au kupotosha tukio hili, kutikisa muungano kabla ya mkutano huo, litapingwa".
Marekani ilitarajiwa kutumia mkutano ujao kumshinikiza zaidi Bw Yoon kutuma silaha kwa Ukraine. Jambo hilo ni nyeti zaidi















