Maangamizi ya nyuklia yanaweza kutokea, Mkuu wa Umoja wa mataifa aonya

Chanzo cha picha, Reuters
"Tumekuwa na bahati isiyo ya kawaida hadi kufikia sasa," alisema Antonio Guterres.
Huku hali ya wasi wasi ikiendelea kutanda duniani, "binadamu ni swala la kutoelewana tu mara moja,kukosea mahesabu tu maramoja kabla yatokee maangamizi ya nyuklia ", aliongeza.
Amezitoa kauli hizo katika ufunguzi wa mkutano wa nchi zilizosaini mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia.
Mkataba huo wa mwaka 1968 ulianzishwa baada ya mzozo wa makombora wa Cuba, tukio ambalo mara kwa mara huelezewa kama wakati ambapo dunia ilikaribia zaidi kuingia katika vita vya dunia kuliko wakati mwingine wowote ule. Mkataba huo uliundwa kwa ajili ya kuzuia kusambaa kwa silaha za nyuklia katika nchi zaidi, na kukamailisha kikamilifu umalizwaji wa silaha za nyuklia.
Karibu kila nchi duniani imesaini mkataba huo unaofahamika kama NPT, zikiwemo nchi tazo zenye nguvu zaidi za nyuklia. Lakini miongoni mwa mataifa kadhaa ambayo hayakuwahi kamwe kusaini ni maane ambayo yanaaminiwa au kushukiwa kuwa na silaha za nyuklia: India, Israel, Korea Kaskazini na Pakistan.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Guterres alisema kuwa "bahati" ambayo dunia imeifurahia hadi sasa ya kuepuka maafa ya nyuklia huenda isidumu- na akaitaka dunia kuangalia upya jinsi ya kuongeza juhudi za kumaliza silaha za aina hiyo.
"Bahati sio mkakati. Wala sio kinga ya kuwepo kwa ongezeko la wasi wasi wa siasa za kieneo zinazoweza kusababisha mzozo wa nyuklia," alisema.
Ameonya pia kwamba wasi wasi huo wa kimataifa "unafikia viwango vya juu " – akielezea hususan uvamizi wa Ukraine, mzozo kuhusu Rasi ya Korea na katika Mashariki ya Kati, kama mifano.
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Urusi ilishutumiwa na wengi kwa kuendeleza wasi wasi wakati wakati siku kadhaa baada ya uvamizi wa Ukraine katika mwezi Januari , Rais Vladimir Putin paliviweka vikosi vya nyuklia katika hali ya tahadhari.
Pia alitishia kuwa yeyote atakayeipinga njia ya Urusi atapata athari "ambayo haujawahi kuyashuhudia katika historia yako". Mkakati wa nyuklia wa Urusi ni pamoja na matumizi ya nyuklia iwapo uwepo wa taifa utakabiliwa na tisho.
Jumatatu, Bw Putin aliuandiakia mkutano huo wa udhibiti wa silaha za nyuklia ambao ulifunguliwa na Bw Guterres, akitangaza kwamba "hapawezi kuwa na washindi katika vita vya nyuklia na havipaswi kamwe kuanzishwa".
Lakini Urusi bado imejipata ikikosolewa katika mkutano wa NPT.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alilaani kile alichokiita Ubabe wa Urusi – na kuelezea kwamba Ukraine ilikuwa imekabidhi silaha zake za nyuklia baada ya enzi ya Muungano wa Usovieti mwaka 1994, baada ya kupokea hakikisho la usalama wake wa siku zijazo kutoka kwa Urusi na wengine.
"Hii inatuma ujumbe gani kwa nchi yoyote duniani ambayo inaweza kufikiria kuwa inahitaji kuwa na silaha za nyuklia - kulinda, kuzuia uchokozi dhidi ya uwepo wake na uhuru? "aliuliza. "Ujumbe ambao huenda ni mbaya zaidi ".
Leo, silaha za nyuklia 13,000 zinazodhaniwa kuwa zinaweza kutumiwa katika maghala ya silaha katika nchi zenye silaha za nyuklia - kiwango ambacho ni cha chini sana kuliko idadi iliyokadiriwa ya lundo la 60,000 katika miaka ya katikati ya -1980 .















