Muswada wa Ghana wa kupambana na LGBTQ+ ni nini?

Chanzo cha picha, Getty Images
Thomas Naadi, Esther Ogola & Beryl Munoko
BBC News Accra, Nairobi na London
Mswada tata wa Ghana dhidi ya LGBTQ umepitishwa na bunge lake kufuatia mjadala na kusomwa kwa mara ya tatu bungeni.
Sheria hiyo mpya inamaanisha kuwa raia wa Ghana wanaojitambulisha kama LGBTQ+ watafungwa jela hadi miaka mitatu.
Bunge la Ghana kwa kauli moja lilipitisha ripoti ya kamati iliyopewa jukumu la kupitia upya mswada huo na kutoa mapendekezo. Hata hivyo, Kiongozi wa Wengi Alexander Afenyo-Markin alikubaliana na kifungo cha jela kwa ngono ya mashoga na wahamasishaji wa LGBTQ +. Alisema kuwa njia bora zaidi ni huduma ya jamii badala yake.
Mswada huo, ambao hapo awali ulipewa jina la 'kukuza haki sahihi za kijinsia za binadamu na maadili ya familia ya Ghana' uliwasilishwa kwa mara ya kwanza bungeni mnamo 2021. Ilisababisha malalamiko ya ndani na ya kimataifa kutoka kwa mashirika ya haki za binadamu.
Kwa nini mswada huo uliwasilishwa?
Mapenzi ya jinsi moja yamekuwa ya kosa la jinai nchini Ghana, hata hivyo, wabunge wanaounga mkono sheria ya sasa wanasema mswada uliandaliwa kwa lengo la kujibu moja kwa moja kufunguliwa kwa kituo cha utetezi wa LGBTQ + nchini, mnamo mwezi wa Januari 2021.
Baraza la Taifa la Machifu, Imamu Mkuu wa Taifa, Muungano wa Kitaifa wa Haki za Kijinsia na Maadili ya Familia, miongoni mwa mashirika mengine ya kidini, walilaani kufunguliwa kwa kituo hicho, na kutaka kifungwe na wale waliohusika washtakiwe.
Walisema kituo na shughuli pana za LGBTQ + nchini haziendani na maadili ya Ghana na kwamba sheria zinazoelezea shughuli za LGBTQ + zinapaswa kuimarishwa.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kamati ilipendekeza nini kuhusu muswada huo katika ripoti yake?
Wakati muswada huo ulipowasilishwa bungeni kwa mara ya kwanza ulilaaniwa sana na kulikuwa na malalamiko kadhaa. Ilipelekwa kwa kamati ya kikatiba, kisheria na bunge ya Ghana kujumuisha wasiwasi kutoka kwa umma.
Wakati kamati ilipopendekeza muda wa kifungo cha jela upunguzwe, mahusiano ya LGBTQ + na shughuli zinazohusiana - ikiwa ni pamoja na kitu chochote ambacho kinaweza kuchukuliwa kama kukuza haki za LGBTQ + - bado ni uhalifu.
Bunge halikuchapisha ripoti ya kamati hiyo, lakini nyaraka ambazo BBC ilizishuhudia zilielezea mapendekezo yaliyotolewa, ikiwa ni pamoja na:
- Kutambua LGBTQ + kuwa haramu na atakayepatikana na hatia kukabiliwa na kifungo cha miaka mitatu (hii imepunguzwa kutoka kwa kipindi cha miaka mitano kilichopendekezwa awali).
- Fedha au udhamini wa shughuli za LGBTQ + itakuwa kinyume cha sheria na kubeba kifungo cha miaka mitano (hii imepunguzwa kutoka miaka 10 iliyopendekezwa awali).
- Kuunda kikundi chochote cha LGBTQ +, jamii, chama, klabu, au shirika, itakuwa haramu na kosa litaadhibiwa kwa hukumu ya juu ya miaka mitano (hii imepunguzwa kutoka miaka 10).
- Umma utahimizwa kuripoti wanachama wa jamii ya LGBTQ + kwa mamlaka 'kwa hatua muhimu'. Kutakuwa na kifungo cha hadi miaka 10 kwa utetezi wa LGBTQ + na kueneza mapenzi hayo kwa watoto, wakati utetezi au msaada kwa masuala ya LGBTQ +, utaadhibiwa kiwango cha juu cha kifungo cha jela cha miaka mitano.
- Kifungu chenye utata sana kinachotetea tiba ya msongo wa mawazo kimeondolewa.
- Maneno mengine pia yalibadilishwa - kwa mfano, neno amorous, linalohusiana na kuonyesha maonyesho ya umma ya mapenzi, lilibadilishwa kuwa la kimapenzi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Majibu yalikuwa yapi?
Shirika la Amnesty International liliupinga mswada huo, likisema kuwa ulichochea chuki dhidi ya watu wanaojitambulisha kama LGBTQ+.
Umoja wa Mataifa uliuelezea mswada huo kama wa kibaguzi - kwa kuwatia hatiani watu wanaojitambulisha kama LGBTQ+.
Mashirika mengine ya kutetea haki za binadamu pia yamelaani vikali hatua hiyo. Tume ya AIDs ya Ghana ilielezea wasiwasi kwamba mafanikio yoyote yaliyopatikana ili kuzuia na kutokomeza magonjwa kama vile VVU yatarejeshwa kwa sababu ya hofu ya usalama kutoka kwa wanachama wa jamii ya LGBTQ +.
Baadhi ya taasisi na watu binafsi pia wameelezea wasiwasi wao kwamba muswada huo unaweza kuwa na athari mbaya kwa uhusiano wa kidiplomasia, baina ya nchi mbili na wa kimataifa kati ya Ghana na nchi nyingine, hasa washirika wa Ulaya katika eneo la biashara.
Je, mswada huo utaathirije jamii ya wapenzi wa jinsi moja na LGBTQ+ kwa ujumla?

Wakati kuacha tiba ya msongo wa mawazo ni muhimu, adhabu kali zilizoainishwa katika muswada huo inamaanisha kutambua kama LGBTQ + imepigwa marufuku. Kusaidia na kuchapisha nyenzo zinazoonekana kama kukuza ajenda ya LGBTQ + pia zimefanywa kuwa haramu.
Ikiwa sheria hiyo itaanza kutumika, wanaharakati wanasema wanachama wa jamii ya LGBTQ+ wataishi mafichoni. Pia kuna hofu ya uwindaji wa wachawi dhidi ya wanachama wa jamii ya LGBTQ + na wale wanaofanya kampeni kwa haki zao nchini Ghana.
Waandishi wa habari pia wanaweza kuwa katika hatari ikiwa ripoti za habari zinachukuliwa kuwa za pro-LGBTQ +, ingawa taarifa zitalindwa chini ya uhuru wa uhuru wa vyombo vya habari vilivyohakikishiwa katika katiba.

Nini kitatokea baada ya hapo?
Sasa kwa kuwa mswada huo umepitishwa, utakuwa sheria tu ikiwa utasainiwa na Rais Nana Akufo Addo, anaweza hata hivyo kuamua kutoidhinisha sheria hiyo ikiwa anadhani utekelezaji utakuwa ghali sana.














