Kwa nini kanisa la Kiafrika linaipinga Vatican kuhusu suala la mapenzi ya jinsi moja?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Taarifa ya kwamba Vatcan imeidhinisha baraka kwa wenzi wapenzi wa jinsia moja iligonga vichwa vya habari na kurasa za mbele za vyombo vyote vya habari hususan vya kimataifa.

Uamuzi wa kihistoria ambao uliwashangaza Wakristo wengi wa Kikatoliki duniani kote. Hata hivyo, kulingana na Profesa Jean-Paul Messina, mtaalamu katika Historia ya Ukristo, "kwa watazamaji, ilikuwa inatabirika".

Mwalimu katika Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afrika ya Kati anaonyesha kwamba kulikuwa na sinodi juu ya familia iliyodumu kwa miaka miwili na ambayo ilifichua "tofauti kubwa kati ya Uaskofu wa Magharibi na Uaskofu wa Kiafrika, haswa kwa sababu ya kile kinachoitwa umakini wa kichungaji ambao ulilazimika kutekelezwa hasa kwa wapenzi wa jinsia moja na watu waliotalikiana au waliofunga ndoa tena.”

Hilo lilitetewa na Papa Francis ambaye tayari alikuwa amewaudhi maaskofu kadhaa kutoka Afrika na kwingineko. Walihisi kwamba nchi za Magharibi zilitaka kulazimisha maono yake ya mapenzi ya jinsi moja kwa Waafrika.

Hakika, tangu kuchaguliwa kwake mwaka wa 2013, Papa Francis amejaribu kufanya Kanisa kuwakaribisha watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsi moja na LGBTQ+ kwa ujumla, bila kubadilisha mafundisho ya maadili.

Mnamo Julai 2013, tayari alitoa sauti ya upatanisho kwa wapenzi wa jinsia moja kwa kutangaza: "Ikiwa mtu ni mpenzi wa jinsi moja na anamtafuta Bwana kwa nia njema, mimi ni nani nimhukumu?"

Kwa hivyo Papa Francis alipinga unyanyapaa wa watu wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.

Miaka kumi baadaye, mnamo Julai 2023, Papa mkuu aliinua gia kwa kufungua mlango, katika barua iliyotumwa kwa makadinali wahafidhina, kwa idhini ya baraka kwa wapenzi wa jinsia moja na watu waliotalikiana.

Pia tunakumbuka kwamba Novemba mwaka jana Vatcan ilikuwa tayari imeidhinisha ubatizo wa waumini waliobadili jinsia na waumini wengine wa jamii ya LGBTQ katika Kanisa Katoliki.

Ilibainishwa kwamba waamini waliobadili jinsia "wanaweza kupokea ubatizo, chini ya hali sawa na waamini wengine, ikiwa hakuna hali ambayo kuna hatari ya kusababisha kashfa ya umma au kutokuwa na uhakika kati ya waaminifu."

Tarehe 18 Desemba 2023, tamko la azimio la muongozo wa mafundisho na maadili ya Wakatoliki “ Fiducia supplicans” kuhusu maana ya kichungaji ya baraka, lililochapishwa na dicastery (huduma) ya Mafundisho ya Imani na kuidhinishwa na Papa, hatimaye liliidhinisha mradi wa zamani.

w

Chanzo cha picha, Getty images

Maelezo ya picha, Baba Mtakatifu Francisko anaongoza Ibada ya Misa Takatifu ya kumbukumbu ya Hayati Baba Mtakatifu Benedikto XVI na Makardinali na Maaskofu waliofariki dunia mwaka 2023.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kulingana na Vatcan, tamko la " Fiducia supplicans " ni jibu kwa ombi la watu wawili la baraka, hata kama hali yao ya uhusiano ni "isiyo ya kawaida."

Hati hiyo ya kurasa nane inabainisha kwamba namna ya baraka “haipaswi kupangwa kidesturi na wenye mamlaka wa kikanisa ili kuepuka mkanganyiko wowote na baraka mahususi kwa sakramenti ya ndoa.” Ni lazima ifanyike "nje ya liturujia".

Mkuu wa Mafundisho ya Imani ya kikatoliki, Kardinali Victor Ferandez anaeleza kuwa "fundisho la ndoa halibadiliki na baraka haimaanishi kuidhinishwa kwa muungano."

Kwake yeye, ibada na sala ambazo zinaweza kuleta mkanganyiko kati ya kile kinachojumuisha ndoa na kile kinachopingana ni "hazikubaliki".

"Waombaji wa Fiducia" wanakumbuka kwamba, kulingana na "mafundisho ya kudumu ya Kikatoliki", ni mahusiano ya ngono tu ndani ya mfumo wa ndoa kati ya mwanamume na mwanamke yanachukuliwa kuwa halali.

Baraka za wale wanaoitwa wanandoa wasio wa kawaida na wa jinsia moja lazima hazipaswi kujumuishwa katika sakramenti ya ndoa ya jinsia tofauti.

Hata hivyo, Vatcan inatoa uchaguzi huru kwa makuhani kuamua kwa msingi wa kisa kwa kisai na "hawapaswi kuzuia ukaribu wa Kanisa na watu katika hali yoyote ambapo wangeweza kuomba msaada wa Mungu kwa njia ya baraka rahisi ".

Kauli hiyo ya utata ilileta ilileta mkanganyiko haraka kati ya waumini wa Kikatoliki na kulaaniwa vikali na makasisi wa Kiafrika.

Baraka ambayo inagawanya

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Papa Francis katika Kanisa Kuu la Notre-Dame du Kongo huko Kinshasa, DRC, tarehe 2, Februari, 2023.

Badala ya kutoa ufafanuzi juu ya utaratibu wa kubariki Kanisa Katoliki, "Fiducia supplicans" badala yake wameibua upinzani mkali kutoka kwa maaskofu wengi hasa barani Afrika.

Karibu kwa kauli moja, maaskofu wa Kiafrika waliitikia kwa ukali fulani ambao si kawaida kwao.

Upinzani huo ulipamba moto hasa katika nchi za Malawi, Nigeria na Zambia pamoja na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika taarifa yake lililochapishwa Jumamosi, Desemba 23, Baraza la Kitaifa la Maaskofu wa Congo (CENCO) lilisema kwa uwazi "hapana kwa aina yoyote ya baraka za wapenzi wa jinsia moja."

Katika ufafanuzi huo huo, CENCO inapendekeza kwa mapadre waliowekwa rasmi, makatekista na wahuishaji wa kichungaji "wasitoe baraka kwa wanandoa wanaume na wanawake, hata wale walio imara, lakini katika hali isiyo ya kawaida". Kwa makasisi wa Congo, baraka kama hiyo inaweza kusababisha kuchanganyikiwa na kuingizwa kwa sakramenti ya ndoa.

Kwa maaskofu wakuu na maaskofu wa Ivory Coast tamko la " "Fiducia supplicans" " limepanda "kuvurugika kwa watu wa Mungu".

Katika tamko lililotiwa saini tarehe 27 Desemba na Mgr Marcellin Yao Kouadio, rais wa baraza la Maaskofu wa Kikatoliki wa wa Ivory Coast (CECCI), walithibitisha tena "kiambatisho chao kwa maadili ya familia, ya sakramenti ya ndoa kati ya mwanamume na mwanamke, kama Mungu alivyomtaka tangu mwanzo. Hii ndiyo sababu Mgr Marcellin Yao Kouadio aliwataka "Wahudumu waliowekwa rasmi kujiepusha na baraka za wapenzi wa jinsia moja na wanandoa katika hali isiyo ya kawaida".

Mwitikio sawa kutoka kwa Baraza la Maaskofu la Maaskofu wa Cameroon. Rais wake, Bw Andrew Fuanya Nkea, anaona mapenzi ya jinsi moja ni "ugeni ambao unadhuru sana ubinadamu. Kwa sababu hautokani na thamani yoyote maalum kwa wanadamu, ni kudhoofisha utu wa upendo, na chukizo."

Huku wakirejelea "kukataa kwao mapenzi ya jinsi moja na miungano ya watu wa jinsia moja", Maaskofu wa Cameroon "wanakataza rasmi baraka zote za wapenzi wa jinsi moja katika Kanisa la Cameroon."

Huko Senegal, Askofu Mkuu wa Metropolitan wa Dakar, Monsinyo Benjamin Ndiaye, ndiye aliyebeba sauti ya wenzake. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, maaskofu wa Senegal wanasema hawapitishi "hukumu kwa watu" lakini "wanakemea mpango wowote wa kutaka kuhalalisha mapenzi ya jinsi moja ambao hauambatani na maadili yetu ya jadi, hata kidogo na imani zetu za kidini za Kikristo".

Nchini Kenya, kanisa lenye busara lilianzishwa ili kuwakaribisha waabudu wa LGBT Desemba 21, 2023

Profesa Jean-Paul MESSINA anaelezea hisia hizi kwa mtazamo maradufu tulionao kuhusu mapenzi ya jinsi moja barani Afrika.

Kulingana naye, tuna hisia kwamba katika Afrika, "mapenzi ya jinsi moja yanahusishwa na mamlaka na kwamba hii itakuwa ni kitamaduni wa mapenzi ya jinsi moja".

Mtaalamu huyo wa masuala ya kidini anaongeza kwamba kwa kweli, si aina ya “ngono iliyoidhinishwa na inayopendwa na watu wengi” katika mila zetu nyingi kama inavyofanywa katika nchi za Magharibi.

Katika Afrika, "mapenzi ya jinsi moja huonekana kama njia ya kufanya uchawi".

Mabaraza mbalimbali ya Maaskofu wa Afrika yamebakia ndani ya mtazamo wa uhafidhina ambao unatetea baraka ya ndoa kwa ajili ya kuendeleza jamii ya binadamu, anaamini Léopold Sédar Edong, mwalimu-mtafiti na mtaalamu wa ustaarabu na dini.

Pamoja na wito huu wa msingi wa ndoa kulingana na Maandiko Matakatifu, Maaskofu Waafrika pia wanaathiriwa na utamaduni wao wa Kiafrika.

Dk Léopold Sédar Edong anaongeza kwamba makasisi wa Kiafrika wana "wajibu maradufu mbele ya Kristo na mbele ya mababu, mbele ya ardhi ya Afrika". Hili ndilo linalohalalisha kutoamini kwao.

Kutuliza dhoruba...

Baada ya kilio kilichosababishwa na tamko la Disemba 18, Vatican ilijaribu mnamo Januari 4, 2024 kuwatuliza maaskofu wa Kikatoliki wa nchi fulani waliokataa kuidhinisha baraka za wapenzi wa jinsia moja.

Daktari ilisema kuwa vatcan ilitaka kufafanua tamko hilo ikipendekeza usomaji kamili na utulivu.

“Ikiwa kuna sheria zinazoshutumu kitendo rahisi cha kuja gerezani kuwa ugoni-jinsia-moja na, katika visa fulani, kuteswa, na hata kifo, ni wazi kwamba baraka haitakuwa jambo la hekima,” ilisema Vatcan.

Hata hivyo, Holy See haina nia ya kuacha mradi huu wa kuwabariki wapenzi wa jinsi moja na wanandoa katika hali isiyo ya kawaida.

Katika maelezo yake ya ziada na ya maelezo kwa Fiducia Supplicans, inatambua kwamba katika "nchi tofauti kuna maswali yenye nguvu ya kitamaduni, hata ya kisheria, ambayo yanahitaji muda na mikakati ya kichungaji ambayo huenda zaidi ya muda mfupi." Kwa maneno mengine, ibada hii ya baraka itafanywa hatua kwa hatua na kulingana na muktadha.

Licha ya ufafanuzi huu, maaskofu wa Kiafrika bado hawako tayari kutoa fursa ya "umakini wa kichungaji" kwa wapenzi wa jinsia moja kama ilivyopendekezwa na Papa.

Kulingana na Profesa Messina, Papa yuko kwenye uwanja wa uchungaji wakati barani Afrika, tunajikuta kwenye "uwanja ambao wakati huo huo ni wa kijamii, jadi na wachungaji".

Mgawanyiko unawezekana?

f

Chanzo cha picha, Getty images

Maelezo ya picha, Baba Mtakatifu Francisko wakati wa hadhara kuu katika Ukumbi wa Paul VI tarehe 3 Januari 2024.

Ndani ya Kanisa Katoliki, maoni yamegawanyika. Upande mmoja tuna wahafidhina wanaokataa kubariki ndoa zisizo za kawaida na kwa upande mwingine wanamageuzi wanaodai kwamba ulimwengu na Kanisa vinaweza kubadilika kwa kukubali jumuiya za wapenzi wa jinsi moja na jinsia nyingine katika LGBTQ kwa ujumla.

Kwa Dk. Edong, upinzani huu wa kimafundisho tayari unajumuisha "mgawanyiko wa kiitikadi" hata kama bado hatuna mgawanyiko rasmi.

Ili kuondokana na kutoelewana huku kwa kitheolojia, Profesa Messina anapendekeza kupangwa kwa sinodi inayoongozwa na Papa ili kudhibiti suala la mapenzi ya jinsi moja ndani ya kanisa na kutatua tofauti zilizopo kuhusu suala hili. Hii, huku ikizingatiwa kuwa "kitamaduni suala la wapenzi wa jinsi moja barani Afrika halikubaliki".

Wachunguzi kadhaa wanaamini kwamba Kanisa Katoliki linajikuta katika njia panda. Kama vile mikutano kadhaa ya Maaskofu imekaririri kuwa baadhi ya waamini wamechanganyikiwa na wana mashaka.

Kufikia Oktoba 2022, Afrika ilikuwa na Wakatoliki milioni 256, au karibu 18% ya wakazi wa bara hilo kulingana na takwimu za Vatcan.

Kufikia mwaka wa 2050, mataifa matatu barani Afrika yatakuwa miongoni mwa mataifa makubwa zaidi ya Kikatoliki duniani.

Ingawa Afrika inachukuliwa kuwa "mustakabali wa Kanisa Katoliki", likikabiliwa na kuongezeka kwa makanisa ya kiinjili na yanayoitwa uamsho, linaweza kupoteza wafuasi.

Unaweza pia kusoma:

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi na kuhaririwa na Ambia Hirsi