Wafahamu makocha 5 wa Afrika wanaoongoza timu zao katika kombe la Dunia Qatar

Na Abdalla Seif Dzungu

BBC Swahili

.
Maelezo ya picha, Makocha wanne wa Afrika kuongoza ti,mu zao kombe la Dunia Qatar

Cameroon, Ghana, Morocco, Senegal na Tunisia zitawakilisha bara Afrika kwenye kombe la Dunia nchini Qatar. Je, wajua kuwa kati ya timu hizi 5, 4 zina makocha wa kutoka Afrika?

Mnamo mwaka wa 2014, Stephen Keshi alikua kocha wa kwanza Mwafrika kuipitisha timu ya Afrika katika raundi ya kwanza ya Kombe la Dunia, jambo ambalo Cisse, Kadri, Regragui, Song, na Addo wanaweza kuiga.

Bila shaka Mataifa yote yatakuwa yakitafuta kuweka historia chini ya ukufunzi wa makocha hawa.

Swali ni je unawafahamu makocha hawa na uzoefu walio nao katika safu ya soka?

Rigobert Song - Cameroon

.

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha, Rigobert Song

 Rigobert song ni mchezaji wa zamani wa Cameroon ambaye ndiye mkufunzi mpya wa timu ya taifa ya indomitable lions. Rigobert Song anayejulikana kwa uzoefu wake wa kiwango cha juu katika safu ya ulinzi alikua mchezaji wa Liverpool na Westham nchini Uingereza kabla ya kuhamia Uturuki ambapo aliichezea timu ya Galatasaray na Trabzonspor.

Kufuatia matokeo mabaya katika michuano ya mataiufa ya Africa AFCON iliyoandaliwa na Cameroon mapema mwaka huu, aliyekuwa mkufunzi a timu ya taifa ya Cameroon Toni Conceicao alifutwa kazi na badala yake Song akapatiwa usimamizi wa timu hiyo . Song anapendelea mbinu ya 4-2-2 uwanjani.

Hatahivyo licha ya kuwa sifa yote inamwendea nguli huyo wa Cameroon kwa mchezo wa mtoano dhidi ya Algeria , bado kuna wasiwasi kuhusu ushawishi wa Samuel Etoo kuhusu maamuzi ya kikosi hicho na mawaidha ya kuwapatia msukumo wachezaji. Katika kinyanganyiro cha kombe la dunia Cameroon ipo katika kundi G Pamoja na Brazil, Serbia na Switzerland.

Otto Addo - Ghana

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Mkufunzi wa Ghana Otto Ado
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Nana Otto Addo ni meneja wa soka wa Ghana na mchezaji wa zamani aliyezaliwa nchini Ujerumani. Kwa sasa ni meneja wa timu ya taifa ya kandanda ya Ghana, na anafanya kazi kama mkufunzi wa vipaji katika klabu ya Borussia Dortmund.

Mkufunzi huyo aliwahi kuzichezea timu za Borussia Dortmund, Hambuuger SV, Maiz 05 katika ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani.

Licha ya kuzaliwa Ujerumani Addo aliichezea timy ya taifa ya soka ya Ghana kwa takjriban miaka saba kuanzia 1999.

Baada ya kushikilia nyadhifa kadhaa na vilabu vya Bundesliga Hamburg, Borussia Monchengladbach na Borussia Dortmund, aliteuliwa na Ghana kama mkufunzi wake mkuu na kuwa jukumu lake kuu la kwanza. Mkufunzi huyo anapendelea mfumo wa 4-2-3-1 uwanjani.

Baada ya kuilaza Nigeria katika mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya mataifa hayo mawili hasimu, Addo atajisifu kwa kuwa na mwanzo mzuri wa kazi yake ya umeneja.

Uongozi wake wa muda mfupi ambao pia umeshuhudia ushindi wa kirafiki dhidi ya Madagascar, Chile na Nicaragua utapitia mtihani mzito nchini Qatar wakati Ghana itakapokutana na Ureno ya Cristiano Ronaldo, adui wa Kombe la Dunia Uruguay, na Korea Kusini waliofuzu nusu fainali 2002.

Jalel Kadri – Tunisia

.

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Jalel Kadri

Jalel Kadri ni kocha wa kandanda wa Tunisia ambaye kwa sasa ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya kandanda ya Tunisia.

Baada ya ya kazi 25 tofauti za ukufunzi wa usimamizi wa timu ambapo hajawahi kukaa mahali pamoja kwa zaidi ya mwaka mmoja mkufunzi huyu sasa anatarajiwa kupitia kipimo kikubwa lkatika kombe la dunia la Qatari.

Mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 50 anayependelea mbinu ya 4-3-3 alipandishwa cheo kutoka kuwa naibu kocha wa klabu ya Mondher Kebaier Januari.

Alicxhukua usimamizi wa Tunisia katika kombe la Afcon na kuoiongoza kuishinda Nigeria katika mkondo wa timu kumi na sita bora.

Huko Qatar, kibarua kitakuwa kigumu wakati miamba hiyo ya Carthage Eagles watakapomenyana na mabingwa watetezi Ufaransa, waliofuzu robo fainali mara mbili Denmark na mabingwa wa Asia 2015 Australia.

Aliou Cisse - Senegal

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Aliou Cisse

Aliou Cissé ni kocha wa soka wa Senegal na mchezaji wa zamani ambaye ni meneja wa timu ya taifa ya Senegal.

Cissé anajulikana zaidi kwa kuwa nahodha wa kwanza wa Senegal kufika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka wa 2002 na meneja wa kwanza wa Senegal kushinda shindano hili mwaka wa 2022 baada ya kufika fainali mwaka wa 2019.

Akiwa ameanza maisha yake ya soka nchini Ufaransa, baadaye alizichezea klabu za Uingereza Birmingham City na Portsmouth. Cissé alikuwa kiungo mkabaji ambaye pia, mara kwa mara, alicheza beki wa kati.

Cissé amekuwa kocha mkuu wa Senegal tangu 2015, baada ya kutimuliwa kwa Amara Traoré, katika nafasi ya meneja mnamo 2012. Pia alikuwa kocha msaidizi wa timu ya vijana chini ya miaka 23 kutoka 2012 hadi 2013, akiwa kocha mkuu kutoka 2013 hadi 2015.

Kwa mbali mafanikio zaidi ya quintet hii. Cisse aliisaidia Senegal kutwaa Kombe lao la kwanza la Mataifa ya Afrika (AFCON) nchini Cameroon mwaka huu.

Msenegali huyo ambaye anapendelea mtindo wa kushambulia wa 4-3-3 kushambuliapia ndiye pekee kati ya watano walio na uzoefu wa Kombe la Dunia kama meneja, baada ya kuiongoza Simba ya Teranga kwenye michuano ya 2018 nchini Urusi.

Mnamo mwaka wa 2018, Senegal ilikaribia kufuzu kwa hatua ya 16, hata hivyo, ilifungwa 1-0 na Colombia, sawa na Japan ambao walishindwa na Poland lakini walifuzu mbele ya Waafrika .

Uchezaji wa Senegal katika miezi ya hivi karibuni umewaacha wengi wakidhani kwamba kikosi cha Cisse kinaweza kuwa timu ya pekee ya Afrika kuweza kuvuka kundi lao huko Qatar, lakini hilo bado litaonekana watakapocheza na wenyeji, Ecuador na Uholanzi.

Walid Regragui - Morocco

.

Chanzo cha picha, Reuters

Walid Regragui ni meneja wa kandanda wa Morocco na mchezaji wa kulipwa aliyestaafu ambaye alicheza kama mlinzi. Ni kocha mkuu wa timu ya taifa ya kandanda ya Morocco.

Akiwa mzaliwa wa Ufaransa, Regragui alikuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Morocco. Klabu alizochezea ni pamoja na Toulouse, AC Ajaccio, Grenoble na Racing Santander.

Katika msimu wa joto wa 2009, alihama kutoka Grenoble hadi timu ya Morocco, Moghreb Tétouan kucheza katika klabu yake ya mwisho .Akiwa mpya miongoni mwa makocha hao watano wa timu za Afrika, Regragui alichukua mahala pake vahid halihodzich – ambaye alidaiwa kuwatenga baadhi ya wachezaji wenye vipaji wa Atlas Lions Agosti mwaka huu.

Walid Regragui ambaye anapendelea mtindo wa kucheza wa 4-3-3 aliisaidia Wydad Casablanca kushinda Ligi ya Mabingwa ya CAF kwa mara ya tatu

Walid Regragui aliisaidia Wydad Casablanca kushinda kwa mara ya tatu katika Ligi ya Mabingwa ya CAF

Ingawa Mmorocco huyo mzaliwa wa Ufaransa anaweza kukosa uzoefu wa timu ya taifa, mafanikio yake ya hivi majuzi akiwa na Wydad Casablanca kwenye Ligi ya Mabingwa ya CAF na Botola Pro ya Morocco ni dalili tosha kwamba anatazamiwa kufanya vizuri akiwa na Altas Lions.

Baada ya mechi mbili pekee za kirafiki dhidi ya Paraguay na Chile, Regragui atalazimika kuonyesha kwamba hajakata tamaa na anafaa kwa kazi hiyo wakati Morocco itakapomenyana na Ubelgiji, Canada na Croatia huko Qatar.