Tetemeko laua watu takribani 162 na kujeruhi mamia ya watu Indonesia

Waokoaji wakiwa wamebeba watoto waliojeruhiwa katika tetemeko la ardhi lililoikumba Cianjur

Chanzo cha picha, EPA

Tetemeko la ardhi limepiga kisiwa kikuu cha Java nchini Indonesia, na kusababisha takribani watu 162 kupoteza maisha na mamia kujeruhiwa, walisema maafisa wa eneo hilo.

Tetemeko hilo la kipimo cha 5.6 lilipiga mji wa Cianjur huko West Java, katika kina cha kilomita 10 (maili 6), kwa mujibu wa Data ya Utafiti wa Jiolojia ya nchini Marekani.

Tetemeko hilo lilisikika katika mji mkuu wa Jakarta ulio umbali wa kilomita 100, ambapo watu katika majengo ya miinuko mirefu walihamishwa.

Maafisa wanaonya kuhusu uwezekano wa kutokea mitetemeko ya ardhi na kusema idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka.

Eneo ambalo tetemeko hilo lilipiga lina watu wengi na kukabiliwa na maporomoko ya ardhi, na nyumba zilizojengwa vibaya.

Waokoaji wamekuwa wakijaribu kuwaondoa watu kutoka kwa majengo yaliyoporomoka, na kufanikiwa kumuokoa mwanamke na mtoto wake mchanga, kwa mujibu wa ripoti za eneo hilo.

Herman Suherman, mkuu wa utawala katika mji wa Cianjur, aliviambia vyombo vya habari vya ndani kuwa takriban watu 46 wamepoteza maisha." Takriban watu 700 walijeruhiwa," aliiambia Kompas TV.

Ruka X ujumbe
Ruhusu maudhui? (Mitandao ya kijamii)

Mkala hii imebeba madhui yaliyotoka kwenye mitandao ya kijamii. Tunaomba ruhusa yako kabla kitu chochote hakija pakiwa, sababu wanaweza wakawa wanatumia Cookies na tekinolojia nyingine. Unaweza ukasoma sera sera ya kutumia cookies katika mitandao ya kijamii kabla ya kukubali. Kutazama maudhui haya chagua accept and continue

Onyo: BBC haihusiki na maudhui ya nje

Mwisho wa X ujumbe

Hapo awali, shirika la habari la AFP lilimnukuu akisema majeruhi wengi ni wamevunjika mifupa kutokana na watu kunaswa na vifusi kwenye majengo.

"Magari ya wagonjwa yanaendelea kutoka vijijini kuja hospitali," alisema. "Kuna familia nyingi katika vijiji ambazo hazijahamishwa."

Video kwenye mitandao ya kijamii zilionesha uharibifu wa nyumba na maduka.

Makumi ya majengo yalikuwa yameharibiwa katika mkoa wa Cianjur, Shirika la Kitaifa la Kukabiliana na Maafa lilisema katika taarifa. Ni pamoja na hospitali na shule ya bweni ya Kiislamu.

Tetemeko hilo lilisikika umbali wa kilomita 100 katika mji mkuu

Chanzo cha picha, EPA

Huko Jakarta, wafanyakazi wa ofisi walikimbia kutoka kwenye majengo katika wilaya ya biashara wakati wa tetemeko hilo, ambalo lilidumu kwa dakika moja.

"Nilikuwa nikifanya kazi wakati sakafu ikitikisika. Nilihisi tetemeko hilo waziwazi. Sikujaribu kufanya lolote kushughulikia hali ilivyokuwa, lakini ilizidi kuwa na nguvu na kudumu kwa muda," wakili Mayadita Waluyo aliliambia shirika la habari la AFP.

Mfanyakazi wa ofisi aitwaye Ahmad Ridwan aliiambia Reuters: "Tumezoea [matetemeko ya ardhi] haya huko Jakarta, lakini watu walikuwa na wasiwasi sasa hivi, kwa hivyo pia tuliogopa."

Matetemeko ya ardhi ni ya kawaida nchini Indonesia. Nchi hiyo ina historia ya matetemeko makubwa ya ardhi na tsunami, na zaidi ya watu 2,000 walipoteza maisha katika tetemeko la Sulawesi la mwaka 2018.

w