Je, viumbe wa ajabu wanaweza kumrejeshea binadamu uhai kwa kutumia kifaa hiki?

Chanzo cha picha, CHUO KIKUU CHA SOUTHAMPTON
Katika mamilioni ya miaka, wanadamu wanaweza kutokuwepo tena
Katika mamilioni ya miaka, wanadamu wanaweza kutokuwepo tena.
Utabiri huu unaweza kuonekana wa kutisha, lakini sio jambo ambalo tunahitaji kuwa na wasiwasi nalo.
Aina nyingi za viumbe hutoweka baada ya muda, na ni jambo la kawaida kwamba jambo hilo litawapata wanadamu siku moja.
Lakini sasa wanasayansi wanaamini kwamba ikiwa siku moja wanadamu wataingia katika historia kama ya dinosaria, wamepata njia ya kuwarejesha.
Wamehifadhi vinasaba vya binadamu katika mfumo wa kumbukumbu za aina tano
Wakitumai kwamba katika siku za usoni mtu au viumbe vya ajabu vitapata kumbukumbu hiyo na kuitumia vinasaba hivyo kuumba binadamu aina nyingine.

Chanzo cha picha, Getty Images
Kumbukumbu isiyofutika
Jopo la wataalamu katika Chuo Kikuu cha Southampton linaloongozwa na Profesa Peter Kazansky limetekeleza mradi huu.
Katika mahojiano na BBC, alielezea namna kumbukumbu hiyo ya vinasaba,inavyofanya kazi.
‘’Vinasaba hivi vyenye ukubwa kama sarafu vinaweza kuhifadhi kiasi kikubwa cha taarifa’’
"Jambo la kushangaza ni kwamba zinaweza kudumu kwa muda mrefu sana, mabilioni ya miaka, bila kuharibika au kupoteza taarifa. Ni kama kuwa na kumbukumbu isiyoweza kufutika kamwe."
"Katika mfumo huu maalum,tumehifadhi vinasaba vya binadamu na maelezo yote muhimu kuhusu sisi ni nani.
Ikimaanisha kwamba katika siku zijazo,viumbe watakaokuwepo au hata wale wa ajabu wataweza kugundua hifadhi hizi na kuzitumia kujifunza kuhusu binadamu, hata wakati jamii ya kibinadamu imetoweka kabisa. Teknolojia hii ni kama mfumo wa wakati unaofaa kuhifadhi maarifa muhimu
Kifaa hiki kikoje?
Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.
Bonyeza hapa kujiunga
Mwisho wa Whatsapp
Jopo la wataalamu katika Chuo Kikuu cha Southampton linaloongozwa na Profesa Peter Kazansky limetekeleza mradi huu.
Katika mahojiano na BBC, alielezea namna kumbukumbu hiyo ya vinasaba,inavyofanya kazi.
‘’Vinasaba hivi vyenye ukubwa kama sarafu vinaweza kuhifadhi kiasi kikubwa cha taarifa’’
"Jambo la kushangaza ni kwamba zinaweza kudumu kwa muda mrefu sana, mabilioni ya miaka, bila kuharibika au kupoteza taarifa. Ni kama kuwa na kumbukumbu isiyoweza kufutika kamwe."
"Katika mfumo huu maalum,tumehifadhi vinasaba vya binadamu na maelezo yote muhimu kuhusu sisi ni nani.
Ikimaanisha kwamba katika siku zijazo,viumbe watakaokuwepo au hata wale wa ajabu wataweza kugundua hifadhi hizi na kuzitumia kujifunza kuhusu binadamu, hata wakati jamii ya kibinadamu imetoweka kabisa. Teknolojia hii ni kama mfumo wa wakati unaofaa kuhifadhi maarifa muhimu
Kifaa hiki kikoje?
Timu ya watafiti iliita mfumo huu wa hifadhi za aina tano kwa sababu inaweza kuonyesha vinasaba kutoka pande mbili na katika namna tatu.
Teknolojia hii ni bora kuliko uchapishaji katika karatasi ya 2D kwa sababu viumbe hivyo vya baadaye vinaweza kuiona kama kitu halisi.
Hifadhi hii inaweza kuduma kwa mabilioni ya miaka pasipo kuharibika.Kwa sasa imeshinda rekodi ya dunia ya Guinness mwaka 2014 kama hifadhi ya data inayodumu zaidi.

Chanzo cha picha, Getty Images
Inaweza kudumu katika barafu au moto na hata kustahimili joto kali la nyuzi 1000.
Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Southampton wanaamini kwamba ikiwa aina nyingine ya viumbe hai itakuta taarifa za vinasaba hivi katika siku zijazo, itakuwa na taarifa za kutosha kuzitumia kuwarejeshea uhai wanadamu.
Kwa sasa haiwezekani kuumba wanadamu kwa kutumia teknolojia. Kwa namna nyingine, binadamu hatokei kwa namna yoyote nyingine isipokuwa kuzaliwa.

Chanzo cha picha, UNIVERSITY OF SOUTHAMPTON
Kidonge cha muda maalum ndani ya pango la chumvi huko Hallstatt, Austria.
Ina ufunguo maalum kwa ajili ya mtu ambaye anaweza kuupata katika siku zijazo.
Vinasaba hivi vitahifadhiwa katika kumbukumbu za binadamu.Ikihifadhiwa maalum ndani ya pango la chumvi huko Hallstatt,nchini Austria.
"Ufunguo huo humpa mtu anayepata ujuzi muhimu kuhusu taarifa iliyohifadhiwa na namna ya kuitumia," anasema Profesa Kazansky.
Imetafsiriwa na Martha Saranga na kuhaririwa na Ambia Hirsi