"Kuna watu wanasema natumia dawa, wananiita mchawi, lakini si kweli" -Mtaalamu wa kushika nyuki

Kutana na kijana Athuman Masimba aka Masimba Nyuki ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kwa kuyahamisha makundi ya nyuki kwa kutumia mikono bila ya nyuki hao kumdhuru.
Athuman amekua akienda sehemu mbalimbali kwa lengo la kusaidia kuhamisha nyuki ambao wangeweza kuleta madhara kwa watu
Baadhi wanaona anatumia nguvu za giza kufanya hivyo, ila yeye anasema ni mapenzi yake kwa wadudu hao ndio yanamfanya wasimdhuru.
Mwandishi wa BBC @mcdavid_nkya_ alikutana nae Mkoani Geita Kaskazini Magharibi mwa Tanzania.









