Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu: Watkins atakiwa Arsenal
Arsenal inataka sana kuwamsajili mshambuliaji wa Sporting na Uswidi Viktor Gyokeres, 27, na mshambuliaji wa RB Leipzig na Slovenia Benjamin Sesko, 22, Lakini ina uwezo wa kumsajili mshambuliaji mmoja tu msimu huu wa kiangazi. (Miror)
Hata hivyo, Arsenal inahisi gharama ya kumsajili Gyokeres iko juu mno hivyo huenda ikaamua kumsajili Sesko au mshambuliaji wa Aston Villa wa Uingereza Ollie Watkins, 29. (Record - kwa Kireno).
Real Madrid inatumai kumsajili beki wa Liverpool Ibrahima Konate, 26, kwa uhamisho wa bila malipo msimu ujao, mkataba wa Mfaransa huyo utakapokamilika. (Marca - kwa Kihispania)
Mshambuliaji wa Manchester United Rasmus Hojlund, 22, ameibuka kama shabaha kuu ya klabu ya Serie A Inter Milan. (Gazzetta dello Sport - kwa Kiitaliano)
Timu hiyo ya Old Trafford imeamua kumbakisha mshambuliaji wa Uholanzi Joshua Zirkzee, 24. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Manchester United ilifanya mawasiliano na wawakilishi wa mshambuliaji wa Ufaransa Hugo Ekitike, 22, anayechezea Eintracht Frankfurt, wikendi hii. (Bild)
Klabu za EPL za Chelsea, Aston Villa na Tottenham zinaendelea kumfuatilia winga wa Manchester United Alejandro Garnacho, 20, baada ya Muargentina huyo kuambiwa yuko huru kuondoka. (Mail)
Klabu ya Al-Hilal ya Saudia imeboresha ofa yake kwa mshambuliaji wa Napoli na anayenyatiwa na Manchester United Victor Osimhen, 26, wakipendekeza mkataba na mshahara wa thamani ya hadi £42.6m kila mwaka. (Goal)
AC Milan imeanza mazungumzo na Arsenal kuhusu usajili wa beki wa The Gunners wa Ukraine Oleksandr Zinchenko, 28. (Corriere dello Sport - kwa Kiitaliano)
Klabu kadhaa za Ligi ya Premia na na Serie A zinamuulizia mshambuliaji wa Bayer Leverkusen wa Czech Patrik Schick, 29. (Sky Germany via Florian Plettenberg)
Paris St-Germain imefikia makubaliano ya kibinafsi na beki wa Bournemouth Illia Zabarnyi, 22, na imepiga hatua ada na klabu hiyo ya Ukraine. (Fabrizio Romano), nje
Galatasaray imewasilisha ombi la kumsajili mlinda lango wa Barcelona mwenye umri wa miaka 33 Marc-Andre ter Stegen. (Sport - kwa Kihispania)
Miamba ya Ureno Porto wanataka kumsajili winga wa Southampton Muingereza Tyler Dibling, 19. (Record - kwa Kireno)
Imetafsiriwa na Ambia Hirsi