Tetesi za Soka Ulaya Jumapili: Manchester City wanapanga kumsajili Paul Pogba

Muda wa kusoma: Dakika 3

Manchester City wanaweza kujaribu kumsajili kiungo wa zamani wa Manchester United Paul Pogba, Newcastle United wanamfuatilia mchezaji wa West Ham Mohammed Kudus, na Bayern Munich kutotafuta mbadala wa Harry Kane mwezi Januari.

Klabu ya Manchester City inatazamia uwezekano wa kumsajili kiungo mshambuliaji i wa Ufaransa Paul Pogba, ambaye anatarajiwa kurejea uwanjani mwezi Machi kufuatia marufuku ya kutumia dawa za kusisimua misuli, lakini inaaminika kuwa mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Juventus mwenye umri wa miaka 31 anasita juu ya kukubali mpango huo wa City.(Independent)

Newcastle United, maarufu kama Magpies wanataka kuchuana na Arsenal na Liverpool katika mbio za kumsajili winga wa West Ham Mohammed Kudus, 24, lakini Magpies watalazimika kuwauza baadhi ya wachezaji wao katika dirisha la usajili la Januari ili kupata fedha za kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana. (Mirror)

Beki wa Liverpool na timu ya taifa ya England Trent Alexander-Arnold, 26, anamaliza mkata wake na klabu hiyo yenye maskani yake katika uwanja wa Anfiled mwishoni mwa msimu huu na amesema hataruhusu mazungumzo na klabu kuhusu mkataba mpya "kujadiliwa hadharani". (Sky Sports)

Alexander-Arnold bado anasalia kuwa lengo kuu la usajili wa Real Madrid mwishoni mwa msimu. Miamba hiyo ya Uhispania pia wanataka kusajili beki mpya wa kati na kuongeza mkataba wa kipa wao namba moja mbelgiji Thibaut Courtois, 32. (Fabrizio Romano via Teamtalk), external

Meneja wa Manchester United Ruben Amorim analenga kufanya usajili wa beki mpya wa kushoto, mshambuliaji na kiungo mshambuliaji ili kuongeza uimara wa wa kikosi chake katika dirisha la usajili la mwezi Januari. (Football Insider), external

Bayern Munich hawatatafuta mbadala wa mshambuliaji wao na nahodha wa timu ya taifa ya England Harry Kane, 31, ambaye ameumia, hayo yamesemwa na mkurugenzi wa ufundi wa klabu hiyo Max Eberl, kuelekea dirisha la usajili la mwezi Januari. (Sky Sports Germany), external

Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza Anthony Gordon amepuuzilia mbali uvumi kuwa alitaka kuondoka Newcastle baada ya msimu uliopita, kabla ya dili la kuhamia Liverpool kushindikana, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 akisema "anafuraha sana" kuwepo katika klabu hiyo yenye maskani yake katika uga wa St James' Park. (Sky Sports), external

Manchester City wana nia ya kumnunua tena beki wa pembeni wa Uholanzi Jeremie Frimpong, 24, kutoka Bayer Leverkusen, miaka mitano baada ya kuondoka katika akademi yao na kujiunga na Celtic. (Football Insider)

Imetafsiriwa na Athuman Mtulya na kuhaririwa na Ambia Hirsi