Je unaweza kujaribu kula Chakula kilichochapishwa cha 3D: ?

www

Chanzo cha picha, Getty Images

Je, ni aina gani ya chakula unapenda zaidi kufungashiwa

Watu wengi wanaweza kuchagua samaki na chips kama chakula chao cha kufungashiwa kwenda kula badae.

Hata hivyo, aina moja ya samaki hasa ya minofu huagizwa na asilimia kubwa ya watu karibia katika kila mgahawa inayotoa huduma ya kufungasha chakula.

Kampuni ya teknolojia ya chakula yenye makao yake makuu nchini Israel inasema imeweza kuchapisha minofu ya samaki iliyo tayari kupikwa au kuandaliwa kwa njia ya kuongeza viungo kadha ili kuleta ladha kwa mara ya kwanza.

www

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Minofu ya samaki iliotengenezwa kwa kutumia seli za samaki wa aina tofauti

Wadau mbali mbali wanaoshughulika na masuala ya chakula ambao wameungana na kampuni ya Nyama ya Umami yenye makao yake makuu nchini Singapore wanasema wametumia seli kutoka kwa samaki wa kundi, ambao hukuzwa na kuwa misuli na mafuta katika maabara.

Samaki iliotengenezwa maabara ya 3D ilitumiwa kuunda minofu, na sahani ya glasi inayoteleza ikiongeza ukubwa wake kwa kila kipande.

Vipande vidogo vidogo vya samaki wanaochukuliwa kama wajadi hutengenzwa kwa ustadi mkubwa na matokea yake huwa ni minofu nyembamba ambayo, wakati wa kuungwa huwa na ladha ya samaki wa baharini.

Je unaweza kula samaki waliotengenezwa maabara aina ya 3D kama kitoweo chako.

Mbadala wa nyama zinazokuzwa katika maabara, kama vile nyama ya ng'ombe na kuku, zimeangaziwa kama njia inayowezekana ya kukabiliana na athari za kimazingira ambazo baadhi ya vyakula tunavyokula huwa nazo kwenye sayari ya dunia.

Kuna wasiwasi kuhusu mchango wa wanyama kama vile ng'ombe linapokuja suala la uzalishaji wa hewa chafu ya ukaa, pamoja na matibabu ya wanyama na athari za shughuli kama vile kilimo kwa mazingira.

Nyama inayotengenezwa kwenye maabara si jambo geni, lakini kufikia sasa, si makampuni mengi ambayo yamejitahidi kutengeneza bidhaa za dagaa zilizochapishwa za 3D ambazo zinaweza kusaidia kulinda idadi ya samaki inayopungua duniani.

Seli-shina za ng'ombe zimechunguzwa kwa kiasi kikubwa lakini mengi zaidi yanajulikana kuhusu samaki, alisema mtendaji mkuu wa kampuni ya chakula ya Umami Mihir Pershad.

"Lazima tujue seli zinapenda kula nini, jinsi zinavyopenda kukua, na hakuna fasihi nyingi za kuanzia," alisema.

Ni lini tunaweza kuanza kuona samaki waliochapishwa wa 3D kwenye migahawa na maduka?

www

Chanzo cha picha, Getty Images

Kwa sasa, mchakato wa kutengeneza samaki waliokuzwa kwenye maabara ni ghali sana ikilinganiswha na bei ya dagaa wa kitamaduni ambao wanaliwa kwa kiasi kikubwa.

Kwa sasa chembechembe za samaki zinazotumiwa hupunguzwa kwa viambato vinavyotokana na mimea katika wino maalum wa kibayolojia unaofaa kwa vichapishi maalum vya 3D.

www

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Samaki wanaokuzwa kwenye maabara huiga sifa za samaki wanaovuliwa baharini na inasemekana ladha yake ni sawa wanapokaangwa na kukolezwa viungo.

"Kadiri muda unavyokwenda, utata na kiwango cha bidhaa hizi kitakuwa cha juu zaidi, na bei inayohusishwa na kuzizalisha itapungua," Arik Kaufman, mtendaji mkuu wa wadau wa masuala ya chakula wanasema kuwa hadi Kufikia sasa, kampuni ya nyama ya Umami imegundua mchakato wa kukuza aina za mimea na mikunga na inatumai kuongeza spishi zingine tatu zilizo hatarini kutoweka kwenye orodha yake inayokua.