Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 02.07.2024
Liverpool inataka kumsajili Anthony Gordon - ingawa Newcastle hawataki kumuuza, huku Manchester United wakitoa mkataba wa miaka mitano kwa Matthijs de Ligt.
Liverpool inamtaka Anthony Gordon ,lakini Newcastle inasisitiza kuwa winga huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 23 hatauzwa. (Telegraph - usajili unahitajika),
Liverpool bado wanavutiwa na Gordon na wanaweza kuchukua hatua nyingine ya kumsajili msimu huu wa joto. (Teamtalk)
Manchester United imempa beki wa Uholanzi Matthijs de Ligt, 24, mkataba wa miaka mitano wakati wakiendelea na mazungumzo ya uhamisho na Bayern Munich . (De Telegraaf - kwa Kiholanzi)
End of Unaweza Pia Kusoma
United watachukua hatua ya kumsajili Jarrad Branthwaite iwapo Everton itapunguza bei ya nyota huyo , lakini The Toffees hawana shinikizo la kifedha kumuuza mlinzi huyo wa England mwenye umri wa miaka 22. (Sky Sports)
Mshambulizi wa Galatasaray Wilfried Zaha ana nia ya kurejea Ligi ya Premia, huku West Ham , Wolves na klabu ya zamani ya Crystal Palace wakimtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast, 31 (Star)
Klabu ya Saudi Pro League inafanya mazungumzo na Newcastle kuhusu mkataba wa kumnunua mshambuliaji wa Paraguay, Miguel Almiron, 30. (Sky Sports)
Arsenal wameanzisha chaguo la kumsajili kipa wa Uhispania David Raya, 28, kutoka Brentford kwa mkataba wa kudumu baada ya muda wa mkopo msimu uliopita.(Mail)
Liverpool na AC Milan wana nia ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot kufuatia kumalizika kwa kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 huko Juventus. (Calciomercato - kwa Kiitaliano)
Sevilla wako tayari kumsajili kiungo wa kati wa Arsenal na Ubelgiji Albert Sambi Lokonga, 24, kwa mkopo wa msimu mzima.(Teamtalk)
Southampton wako tayari kutoa dau la pauni milioni 20 kumnunua kiungo wa kati wa Celtic na Denmark Matt O'Riley mwenye umri wa miaka 23. (Talksport),
Brighton, Brentford, Everton na Southampton wanavutiwa na kiungo wa kati wa Millwall Muingereza Josh Stephenson, 18. (Football Insider)
Newcastle United wamejitolea kusalia na mshambuliaji wa Uswidi Alexander Isak huku kukiwa na ripoti zinazomhusisha mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 na uwezekano wa kuhamia Arsenal au Chelsea .(Football London)
Manchester City wameipiku Arsenal kumpata kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Ryan McAidoo, 16 (Mirror)
Nottingham Forest wanatarajiwa kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Lewis O'Brien msimu huu wa joto huku Sheffield United, Preston North End na Ipswich Town zikimtaka mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25. (Northamptonshire Live)
End of Unaweza Pia Kusoma
Imetafsiriwa na Yusuf Jumah