Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 21.11.2022
Tottenham inamfuatilia winga wa Everton na England U21 Anthony Gordon, 21, kabla ya dirisha la usajili la Januari. (Football London)
Kiungo wa kati wa zamani wa England Alex Oxlade-Chamberlain, 29, anatarajiwa kuondoka Liverpool kama mchezaji huru msimu wa joto. (Fabrizio Romano)
The Reds walitaka kumuuza kiungo huyo kwa £10m msimu uliopita wa joto lakini hawakuweza kukubaliana na klabu nyingine yoyote. (Mirror)
Kiungo wa kati wa Barcelona na Uholanzi Frenkie de Jong, 25, anasema klabu hiyo ya La Liga ilihusika kufichua maelezo ya mkataba wake kwa vyombo vya habari. (De Telegraaf, via Mirror)
Borussia Dortmund haitamuuza mchezaji anayesakwa na West Ham na Leeds Raphael Guerreiro, 28, kabla ya mkataba wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Ureno kukamilika mwishoni mwa msimu huu. (Bild)
Chelsea wana wasiwasi kuwa Romelu Lukaku kutocheza kwenye Kombe la Dunia kunaweza kuathiri thamani ya mshambuliaji huyo wa Ubelgiji mwenye miaka 29 watakapojaribu kumuuza baada ya kumaliza mkopo wake wa msimu mzima katika klabu ya Inter Milan. Lukaku ameondolewa kwenye mechi mbili za kwanza za nchi yake. (Evening Standard)
Manchester United wanakaribia kumpa mshambuliaji kinda wa Argentina, Alejandro Garnacho, 18, mkataba mpya wenye thamani ya £50,00 kwa wiki. (Daily Star)
Mkufunzi wa zamani wa Manchester United Lous van Gaal, ambaye sasa ni meneja wa Uholanzi, anasema alitaka kumsajili mshambuliaji wa pembeni wa Senegal na Liverpool Sadio Mane, 30, wakati alipokuwa Old Trafford. (Metro)
Mshambulizi wa zamani wa Liverpool na Barcelona Luis Suarez, 35, alikataa ofa kutoka kwa Gremio kwa sababu raia huyo wa Uruguay atajiunga na klabu ya MLS, meneja wa klabu hiyo ya Brazil amesema. (Bild)
Mshambuliaji wa Austria Marko Arnautovic, 33, amekataa mara kwa mara kujiunga na Manchester United msimu wa joto - ingawa familia yake ilimtaka aondoke Bologna. (Laola1)
Wakala wa kiungo wa Dynamo Moscow na Urusi Arsen Zakharyan ametaja nia ya Chelsea kumnunua mchezaji huyo wa miaka 19 "hadithi tata". (Champion)
AC Milan wanafikiria kumchukua kwa mkopo mwezi Januari winga wa Chelsea Hakim Ziyech, 29, na kumnunua mshambuliaji wa The Blues mwenye umri wa miaka 21 raia wa Albania Armando Broja. (Corriere Dello Sport)
Milan pia wanavutiwa na kiungo wa kati wa Chelsea Muingereza Ruben Loftus-Cheek, 26, baada ya kuonyesha kiwango kizuri dhidi yao kwenye Ligi ya Mabingwa huko Stamford Bridge. (Calciomercato)