Je kuna vyakula ambavyo vinaweza kukushibisha kwa muda mrefu?

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Kuna baadhi ya vyakula ambavyo vinaweza kupunguza njaa yako, lakini je kuna vyakula vinavyoweza kupunguza hamu yako ya kula?.

Gary Frost, Mkuu wa idara ya Lishe na Chakula Imperial College London, anasema kuwa huku baadhi ya tafiti zimeonyesha kuwa baadhi ya vyakula, ikiwemo tangawizi na pilipili, vinaweza kupunguza hisia ya njaa, hili pia linapaswa kuangaliwa.

Vyakula vingi vimetumiwa katika tafiti na athari zake kwa wanyama zinachunguzwa.

Kulingana naye, "watafiti bado hawajafikia matokeo halisi kuhusu ufanisi wa vyakula hivi kwa binadamu ."

Lakini Mary John Luddy, profesa katika Chuo kikuu cha Bowling Green State Ohio, Marekani, anasema kuwa utafiti unachunguza viungo vilivyomo katika pilipili, ambavyo husababisha ukali wake baada ya kuila. Joto la mwili huongezeka na mtu huhisi kuungua mdomoni.

Katika utafiti huu, Bi. Lodi alijaribu kula vkiungo hiki kwa kiwango cha kawaida ambacho binadamu anaweza kukila.

G

Chanzo cha picha, Getty Images

Alianza utafiti huu kwa kuongeza taratibu pilipili kwenye chakula chake cha nyumbani.

Baada ya muda fulani, aliwaalika watu 25 wa kujitolea kushiriki uchunguzi wake katika maabara yake ndani ya nyakati sita na kuwatengenezea supu ya pilipili.

Watu hawa walikuwa wakikaa masaa manne na nusu katika maabara yake baada ya kula chakula ili kubaini hamu yao ya chakula na matumizi ya nguvu.

Baadaye, alikuwa akiwapa supu ya pilipili tena na mara hii walikuwa wakila chakula kadri wanavyotaka.

Kulingana na utafiti huu, washiriki walikula kalori 10 nguvu zaidi ya mara nne baada ya kunywa supu yenye gramu moja ya pilipili.

Washiriki ambao kwa kawaida hula pilipili mara moja tu kwa mwezi walisema walikuwa na kiwango cha chini cha hamu ya chakula baada ya kunywa supu, na ukiwalinganisha na wale ambao walikula pilipili mara tatu kwa wiki hawakuwa na kabisa ya chakula.

Kulingana na Gary Frost, aina hii ya utafiti unaangazia tu athari za muda mfupi za chakula kwa hamu ya kula na sio athari za muda mrefu kwa mwili.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kuhusiana na hili, tafiti nyingine 32, sawa na hizi pia zimeonyesha kuwa kuna ushahidi mkubwa kwamba pilipili kali au chai ya kijani kibichi inaweza kusababisha kupungua kwa hamu ya kula chakula.

Kinywaji kingine ambacho kiliibua tetesi kwamba kinaweza kuzuia hamu ya chakula ni kahawa.

Matthew Schubert, profesa msaidizi katika Chuo kikuu cha California, Berkeley, alitathmini utafiti ambao umekwishafanywa hadi sasa.

Alitaka kujua iwapo kahawa kweli ina vitu ndani yake vinavyoweza kupunguza hamu ya kula chakula au la.

Tafiti kadhaa za aina hii zimeonyesha kuwa unywaji wa kahawa hupunguza kasi ya mtu kuhisi njaa, hii ikimaanisha kuwa hupunguza kasi ya muda wa kuhama kwa chakula kutoka tumboni kuelekea kwenye utumbo mdogo. 

Alikula chini ya kalori 70 katika mto wa sup. Anasema Bi Lodi : "Suala hili linaelezea sula muhimu, ambalo ni kuungua kwa ndani ya mdomo baada ya kula pilipili’’.

Kwa namna yoyote ile, karoli za ziada ambazo mtu yule aliziunguza baada ya kula chakula chenye pilipili ni kidogo sana na hakina ufanisi kwa muda mrefu kwa utumbo mpana.

Getty

Chanzo cha picha, Getty Images

Lakini hakuna utafiti ulioonyesha kwamba unywaji wa kahawa una athari ya kipekee katika mwili na kupunguza hamu ya kula chakula.

 Schubert anasema kwamba iwapo tafiti zijazo zitathibitisha kwamba kahawa hupunguza hamu ya chakula, inaweza kuwa chini ya karoli 100 hadi 200 kwa siku, kiwango ambacho bado kitakuwa ni kidogo sana.

 Katika baadhi ya tafiti, pia ilisemekana kuwa ulaji wa vyakula vyenye nyuzi nyuzi( fiber) huwafanya watu wawe safi kwa muda mrefu, lakini pia hii inaweza kuwa na athari wakati mtu anapokula vyakula hivi kwa kiwango kikubwa.

Frost anasema: " inashauriwa kuwa tule gramu 30 za vyakula vya nyuzi nyuzi( fiber) kwa siku, lakini watu wengi hula gramu 15 za fiber katika chakula chao cha kila siku.

Iwapo tutaongeza kiasi hiki hadi gramu 30, itaathiri hamu yetu ya kula. Lakini athari itatoweka taratibu ."

Pia kuna imani kwamba kuna vyakula vya protini , ambavyo vinasemekana kupunguza hamu ya chakula, lakini Martin Kollmeier, profesa wa afya ya umma na lishe katika North Karolina nchini Marekani, anasema kwamba badala ya kuweka bidii ya kula aina fulani za vyakula ili kupunguza hamu ya kula, ni bora kunywa maji ambayo hupunguza hamu ya kula kwa muda.