Nyumbani na Arteta - maisha ya utotoni, kazi na familia

g

Chanzo cha picha, PA Media

Tumemwona kama mchezaji na tunamfahamu kama meneja, lakini Mikel Arteta ni nani hasa?

Katika wiki ya mwisho ya msimu wa kusisimua wa Ligi Kuu ya Uingereza, meneja wa Arsenal alimualika mwandishi wa BBC Sport Guillem Balague nyumbani kwake kwa mahojiano ya kipekee ya saa moja.

Arteta anazungumza juu ya utoto wake, kazi yake, maisha yake ya familia na Umeneja wake kazi anayoifanya sasa.

Kuhusu maisha ya utotoni ya Arteta na La Masia

Arteta alikulia katika kitongoji kizuri cha Antiguo huko San Sebastian.

"Ninapenda maji, napenda jua na napenda ufuo, na jumuisha mpira wa miguu juu ya hayo..." anasema.

"Hapo ndipo nilitumia saa nyingi za mchana, nikicheza ufukweni nilipokuwa mtoto. Kwangu mimi, ilikuwa mchanganyiko mzuri."

Akiwa na umri wa miaka 14, Arteta alikutana na kipa wa baadaye wa Uhispania na Liverpool Pepe Reina katika siku yake ya kwanza katika Chuo cha mafunzo ya soka cha Barcelona, ​​La Masia. Alikuwa rafiki na kulala chumba kimoja na magwiji wa Barca, Victor Valdez na Andres Iniesta wakiwa vijana.

"Yeye (Reina) amekuwa mmoja wa marafiki zangu wa karibu," asema. "Tulishiriki vitanda vyetu kwa miaka mitatu. Mojawapo ya kumbukumbu nzuri zaidi ambayo ninayo maishani mwangu ni wakati tuliotumia pamoja.

"Tulikuwa tukishindana kwa sababu ilitubidi - kwa sababu sote tulitaka kufika kwenye kikosi cha kwanza - lakini ilikuwa hisia halisi ya familia."

Arteta kuhusu PSG 'mlinzi' Pochettino

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arteta (kulia) alihamia Ufaransa kwa mkopo akiwa kijana

Akiwa na miaka 17, Arteta alihamia kwa mkataba wa mkopo katika Paris St-Germain, ambapo alikutana na Mauricio Pochettino, ambaye alikua kaka mkubwa na rafiki mzuri.

"Mauricio alikuwa kama ngao kwangu - alikuwa akinilinda dhidi ya kila kitu. Alinipa imani na kujiamini sana," Arteta anasema.

"Alikuwa akicheza nyuma yangu na ilikuwa kama kuwa na mtu anayekusukuma mgongoni mwako na kukufundisha na kukusaidia kila wakati. Sikuweza kupata mtu yeyote bora zaidi." [yake]

Kuhusu kuhamia PSG, Arteta anasema: "Ulikuwa uamuzi mgumu. Ndoto yangu ilikuwa kuichezea Barcelona lakini wakati huo ilibidi nifuate uhalisia wa mambo."

Kuhusu 'kuishi au kufa' kwa Arteta huko Rangers

f

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arteta, akiwa na mkewe Lorena, walipokea heshima ya kifahari ya Uhispania - Agizo la Kifalme la Isabella Mkatoliki, kwa huduma za ajabu kwa Uhispania - katika Ubalozi wa Uhispania huko London mnamo Jumatano.
Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Mnamo 2002 Arteta alisaini mkataba wa kujiunga na Rangers, alipoondoka Barcelona.

"Sijawahi kuona hali kama hii - kuangalia jinsi watu hawa wanavyopenda," soka, anasema Arteta kuhusu ziara yake ya kwanza katika Rangers, ambapo walikuwa wakicheza na PSG katika Ligi ya Mabingwa.

"Uamuzi bora zaidi tuliofanya. Ilikuwa ngumu sana - soka tofauti kabisa. Lazima uishi au ufe."

Wakati akiwa katika Rangers, Arteta alikutana na mwanamke ambaye alikuwa mke wake baadaye, Bi Lorena, mkufunzi wa masuala ya maisha, kwenye safari ya kwenda San Sebastian. Sasa wana watoto watatu pamoja.

“Amebadilisha maisha yangu. Amebadilisha mtazamo wangu kuhusu maisha,” anasema.

"Tumepitia hali nyingi, nyingi tofauti, zingine za kuvutia, zingine ngumu sana.

"Nina hisia na yeye kwamba hatuwahi kuchoka. Ninaweza kukaa hapo saa tano, saa 10, kwenda popote duniani na kufurahia na kufurahi na kucheka.

“Katika taaluma yetu huwa tunazungumza kuhusu mhusika mkuu ambaye ni mchezaji au kocha au meneja.

"Lakini vipi kuhusu mtu ambaye yuko karibu na huyo? Na bila huyo hakuna misingi ya kutosha na hakuna nguvu za kutosha za kuwa thabiti."

f

Chanzo cha picha, BBC SPORT

Maelezo ya picha, Arteta akiwa nyumbani na Guillem Balague siku chache kabla ya timu yake kumenyana na Everton katika mchezo wao wa mwisho wa Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu, wakati bado wana nafasi ya kushinda taji.

'Hisia za huzuni ' kuhusu talaka ya wazazi wa Arteta na kuwa "balaa".

Baada ya kuishi Uskochi, Arteta mwenye umri wa miaka 24 alihamia Real Sociedad ya Uhispania kwa matumaini ya kuweka familia yake pamoja baada ya wazazi wake kusema walikuwa wakitalikiana.

“Nilijihisi kuwa na huisia za huzunni na hatia. Sikujua kama hiyo ilikuwa ni kwa sababu yangu na kujaribu kutekeleza ndoto yangu. Ninahisi kuwajibika sana kwa hilo,” anasema.

"Sikuwahi kuhisi kuwa ulikuwa wito sahihi [kurejea Uhispania], lakini nilikuwa na jukumu na nilitaka kuwaunganisha tena wazazi wangu na familia yangu.

“Ilikuwa balaa. Haijawahi kufanya kazi kwa maana hiyo. Sijawahi kuhisi kuunganishwa kwa wakati wowote."

Arteta juu ya 'kupenda kila dakika' huko Everton

Unaweza pia kusoma:

Arteta alijiunga na Everton mwaka wa 2005 kwa pauni milioni 2 baada ya kufanikiwa kwa kupata mkataba wa mkopo kutoka Sociedad.

“Moja kwa moja, unaungana na timu; unaungana na wachezaji; unaungana na wafanyakazi; unaungana na wafuasi. Na hisia hiyo inahitajika,” anasema.

"Unajiamini, unajisikia msisimko kila asubuhi kushuka kitandani na kwenda kwenye mazoezi. Nilipenda kila dakika."

Arteta kwenye 'uelewano wa ajabu' akiwa na Guardiola

h

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha, Arteta alishinda mataji matano ya nyumbani, yakiwemo mataji mawili ya Ligi Kuu ya Uingereza, katika kipindi cha miaka mitatu na nusu akiwa msaidizi wa Pep Guardiola katika klabu ya Manchester City.

Muda mfupi baada ya maisha yake ya uchezaji kuisha, Arteta mwenye umri wa miaka 34 alijiunga na Manchester City kama meneja msaidizi wa Pep Guardiola.

"Tulikuwa na uelewano mzuri wa ajabu," anasema.

"Kwa kutazamana kwa macho tu tulielewana wazi juu ya kile tulichopaswa kukifanya au kile tulichokuwa tunafikiria wakati huo.

"Lilikuwa ni jambo la kuvutia kuwa sehemu ya kitu kipya."

Arteta kuhusu Arsenal - wakati huo na sasa

Arteta aliichezea Arsenal kati ya 2011 na 2016. Alipojiunga mara ya kwanza, alikuwa akiongea kwenye chumba tulivu cha kubadilisha.

Anasema: "Nilianza kuzungumza na nikaanza kuwaunganisha watu wote - 'Njoo, tufanye hivi, nyie'. Nilisisimka sana.

“Nitafanya kila kitu. Nitavunja kila ukuta hapa. Tunapaswa kufanya hili kutokea.", anakumbuka.

Anasema kuhusu kustaafu: "Ilikuwa inafikia hatua ambayo nilikuwa nahisi kupendezwa zaidi na upande wa kufundisha kuliko upande wa kucheza."

Mnamo Desemba 2019 Arteta alikua meneja wa Arsenal.

"Suala lilikuwa la kina zaidi. Suala lilikuwa kwenye mizizi yetu. Yote yalikuwa ni fujo,” anasema.

"Tunahitaji watu wetu. Tunahitaji kuwashawishi kwamba umejitolea na uko tayari kuipeleka klabu hii sehemu tofauti kabisa.”

Arteta alipanda mzeituni mbele ya ofisi yake, kuashiria umri na mizizi ya klabu.

Anasema hivi: “Niliupanda mti huo na kusema, ‘Hii ni zawadi yangu. Sasa unapaswa kuuangalia. Ni kitu kilicho hai. Huwezi kuuacha ife.'

"Mti huo ni kiasi sawa cha miaka katika klabu yetu ya soka - zaidi ya miaka 130.

"Utakuwa huko kila siku. Lazima muuangalie na nyote muwajibika."

Imetafsiriwa na Dinah Gahamanyi