Kutana na wapiganaji wa kigeni wanaojiunga na vita vya Ukraine dhidi ya Urusi

Ukraine imekuwa kwenye vita kwa zaidi ya siku 100. Tangu wakati huo, zaidi ya wanajeshi 20,000 wa kigeni kutoka nchi zaidi ya 50 wamejiunga na vita dhidi ya Urusi

Wao ni nani na kwa nini wanahatarisha maisha yao? Mwandishi wa BBC Olga Malchevska alipata kufika katika moja ya vituo vyao vya siri vya mafunzo.