Ni makundi gani ya mrengo wa kulia yanayomshinikiza Putin kuanza vita vikuu Ukraine?

Tangu kuanza kwa mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine tarehe 24 Februari mwaka huu, Moscow imejaribu kupunguza kiwango cha vita hivyo.

Urusi imelitaja shambulizi hilo kuwa 'operesheni maalum' na mtu yeyote nchini humo ambaye alijaribu kuiita operesheni hiyo kwa jina lingine alikabiliwa na hasira ya utawala huo.

Shirika tawala la Urusi 'Kremlin' lilikuwa linajaribu kuwasilisha mzozo huu kama pambano la muda lenye lengo fupi.

Ilionekana kana kwamba Urusi ilikuwa inajaribu kufifisha mstari unaotenganisha kati ya vita na amani.

Mnamo Septemba 21, wakati Rais Vladimir Putin alitangaza kuwaaajiri wanajeshi wa ziada kwenye hotuba yake, juhudi zake zilionekana wazi. Lakini jinsi Ukraine ilivyoikabili Urusi imebadilisha hali hiyo.

Kwa upande mwengine baadhi ya raia wa Urusi wanapinga shambulio la Ukraine na wameonesha wazi kupinga hatua hiyo ya kuwasajili wanajeshi wa ziada kujiunga na jeshi.

Kwa upande mwengine , wanajeshi wa mrengo wa kulia wanahisi kwamba Urusi inajizuia kufanya mashambulizi Ukraine na kwamba haipaswi kufanya hivyo. Waliitaka Urusi kutekeleza mashambulizi makali dhidi ya miji ya Ukraine na kwamba haipaswi kujizuia kutumia silaha za kinyuklia

Ili kuelewa sera ya Urusi ya vita , ni muhimu kujua je vikosi hivi vya mrengo wa kulia vyenye msimamo mkali ni vikosi gani na uwezo wao ni upi nchini humo

Vita vya Urusi na Ukraine: Matukio ya Jumapili na Jumatatu

  • Yuri Ihnat,msemaji wa jeshi la angani la Ukraine alisema kwamba , jeshi la nchi hiyo lilitungua makombora manne ya Urusi mapema alfajiri. Kulingana na chombo cha Habari cha Interfax -Ukraine, mashambulizi ya makombora hayo yalianza mwendo wa saa saba asubuhi.
  • Usambazaji wa umeme umeathiriwa na kombnora la Urusi dhidi ya miundomsingi muhimu mjini Lviv Magharibi mwa Ukraine. Baada ya shambulio hilo , hakuna umeme katika baadhi ya maeneo yam ji huo.
  • India imepiga kura dhidi ya Urusi ikitaka kufanyika kwa akura ya siri kuhusu suala la Ukraine katika mkutano wa Umoja wa Mataifa .
  • Zaidi ya mataifa 100m ikiwemo India wanataka kura ya wazi kufanyika kuhusu mapendekezo ya Urusi katika mkutano huo wa Umoja wa Mataifa huku kukiwa na shutuma kuhusu mapendekezo ya Urusi kukalia majimbo manne ya Ukraine.
  • Mashambulizi dhidi ya mji mkuu wa Urusi Kiev yameshtumiwa na mataifa mengi duniani. Marekani imesema kwamba Urusi ililenga maeneo ya raia , ikiweno vyuo vikuu na viwanja vya Watoto kuchezea . Marekani imeihakikishia Ukraine kuhusu msaada zaidi.

Makundi ya Urusi yenye msimamo mkali

Hatahivyo, hakuna mtu nchini Urusi anayedai kuwa "anaunga mkono mrengo wa kulia". Lakini utawala wa Vladimir Putin unajumuisha watu tofauti ambao hawaingiliani kila mmoja wao.

Hawa ni pamoja na watu wenye itikadi kali, kutoka kwa Wanademokrasia wa Kitaifa hadi Wanazi mamboleo, wanamgambo wanaojiita 'wazalendo', wanablogu wa kijeshi na wapiganaji wanaounga mkono Urusi kutoka Donbass.

Mojawapo ya majina haya ni Igor Girkin, kiongozi wa Wanamgambo wa Watu wa Donbass, anayejulikana kama 'Strelkov' au 'Shooter'.

Igor Girkin alikuwa Waziri wa Ulinzi wa nchi iliyojiita 'Jamhuri ya Watu wa Donetsk' kwa muda mfupi katika mwaka wa 2014. Vikosi hivi vya kisiasa havina uwakilishi katika bunge la Urusi.

Chama cha Vladimir Zhirinovsky cha Liberal Democratic Party bila shaka kiliaminika kuwa 'nguvu ya watu wenye msimamo mkali' wa miaka ya tisini, lakini baadaye kiliungana na Chama cha Kikomyunisti na kuwa sehemu ya 'upinzani wa vibaraka'.

'Ukuu wa Urusi'

Urusi katika siku zilizopita imeyawekea vikwazo makundi ya wanaharakati wengi wenye mrengo wa kulia ambao inawaona kuwa hatari na ambao wanaweza kusababisha ghasia.

Vyama vingi vya kitaifa vya upinzani vilikuwa haviwezi kujisajili rasmi.

Lakini iwapo makundi hayo hayakuungwa mkono wakati wa utawala wa Putin, yaliruhusiwa kuwepo katika vyombo vya Habari vya Urusi lakini wakapewa masharti kwamba vitakuwa vitiifu kwa Kremlin.

Ijapokuwa idadi ndogo ya makundi hayo yanapinga shambulio la Ukraine hii leo, kwa upande mwengine sauti ya kuiboresha tena Urusi iko juu miongoni mwa makundi haya ya mrengo wa kulia.

Makundi mengi ya wale wanaounga mkono mrengo wa kulia yaliuna mkono tangazo la Putin kuwasajili wanajeshi wa ziada huku wengi wakiitaja kuwa hatua kubwa nao wengine wakiitaja kuwa hatua ndogo ilipochukuliwa na ambayo imepitwa na wakati.

Kuitisha vita katika maeneo tofauti

Mnamo mwezi Machi 2022, wanajeshi wa Urusi walilazimika kutorokea karibu na mji mkuu wa Kyiv ma baada ya hilo , mapungufu ya kijeshi kila eneo yalionesha udhaifu uliopo katika uongozi wa jeshi hilo.

 Waziri wa ulinzi nchini Urusi Segei Shoigu na uongozi wa kisiasa wa taifa hilo ulikoslewa pakubwa kwa mapungufu hayo. Matokeo yake ni kwamba Wanajeshi wa kitaifa wa Urusi waliwasilisha ombi kwa rais Putin kuishambulia Ukraine. Kulingana na yeye, wakati umefika kusitisha operesheni maalum na kuanza vita rasmi.

Utaifa wa Kirusi umegawanywa katika matawi mawili makuu katika ngazi ya itikadi. Tawi la kwanza linahusiana na tamaa ya ubeberu. Wale wanaoamini katika hili wanasisitiza ukuu wa hali ya Urusi.

Itikadi ya kibeberu

Kwa maoni yake, Urusi inapaswa kupanua mipaka yake hadi kiwango ambacho kinakaribia mipaka ya Umoja wa zamani wa Soviet.

Tawi la pili la utaifa wa Urusi linataka kubadilisha 'Shirikisho la Urusi' kuwa 'taifa la Urusi'. Watu wa itikadi hii pia wanataka Urusi iunganishe yale maeneo ambayo inayaona kuwa yake.

 Ingawa watu hawa wanataka kufanya hivi kwa njia ya amani, lakini ikiwa watalazimika kutumia nguvu kwa hili, basi hakuna tatizo juu yake.

Mtazamo wa itikadi hizi zote mbili unaweza kuonekana katika kampeni ya Urusi dhidi ya Ukraine.

Itikadi ya kibeberu ni mtetezi wa sera ya Urusi ya kupanua mipaka, wakati wale wanaozungumzia utaifa wa kitamaduni pia wanasisitiza suala la watu wa Ukraine wanaozungumza Kirusi nchini Ukraine.

Mbadala wa silaha za nyuklia

Lakini pamoja na tofauti zao, makundi haya mawili ya kiitikadi yanakubalian juu ya jambo moja nalo ni kwamba vita hivi lazima wavishinde kwa njia zote, hata ikibidi Urusi itumie silaha za nyuklia dhidi ya Ukraine.

Mwandishi wa gazeti la Russia Today Yegor Kholmogorov anasema, "Ikiwa mtu angelazimika kuchagua kati ya ushindi dhidi ya Ukraine na vita vya nyuklia vya kimataifa, vita vya nyuklia vingependelewa."

Yegor Kholmogorov pia ni mwandishi wa habari anayeunga mkono itikadi ya ubeberu. Amekuwa mpatanishi wa upatanisho kati ya Kremlin na upinzani.

Kwa maneno ya mtetezi wa utaifa wa kitamaduni na mwanaharakati Alexander Khramov, ikiwa Ukraine itashinda vita hivi kwa msaada wa nchi za Magharibi, Urusi itatawanyika katika majimbo mengi madogo na taifa la Urusi litaangamizwa kabisa.

Watu hawa, wakizidiwa na vita hivi, wanazungumza juu ya utakaso kamili wa jamii ya Kirusi na hii hailingani na malengo ya Vladimir Putin.

Bila kujali matokeo ya vita hivi, ni hakika kwamba vitakuwa na athari kubwa kuhusu utulivu wa ndani wa Urusi.