Afya: Je, kutoa gesi tumboni kuna faida gani kwa afya?

X

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Gesi inayotoka tumboni kiasili ina harufu au kelele. Hata hivyo, kuitoa kumethibitishwa kuwa na manufaa kwa afya.

“Gesi ya tumboni ni mrundikano wa gesi kwenye njia ya usagaji chakula. Tunaposema kutoa gesi ni afya, ni kusema kutotoa gesi kunamaanisha njia kufunga" anaeleza ” anasema Daktari Prince Igor Any Grah, kutoka Ivory Coast.

Baada ya mlo mwili huchagua kila kitu ambacho mwili unahitaji na vingine hugeuka kuwa gesi, na gesi ndani ya tumbo inapaswa kutolewa.

Ni muhimu kuondokana na gesi ili kuwezesha kile tunachokiita mfumo wa kubadilisha chakula kuwa nishati mwilini kufanyika vizuri.

Mtu yeyote mwenye afya anapaswa kutoa gesi tumboni bila kizuizi kwa sababu kutoitoa kunaweza kuwa chanzo cha matatizo ya usagaji chakula.

Pia unaweza kusoma

Chanzo cha gesi

kj

Chanzo cha picha, GETTY IMAGES

Kutoa gesi huonyesha kuwa tumbo linafanya kazi vizuri. Kwa siku, mtu mwenye afya nzuri hutoa gesi kwa wastani wa mara 12 hadi 25.

Gesi ya tumboni hutoka katika vyanzo viwili; hewa iliyomezwa na gesi inayozalishwa na bakteria kwenye utumbo.

"Kutotoa gesi ni tatizo na hilo hukuza kile tunachokiita uvimbe wa tumbo," anaeleza Dk Any Grah.

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Kulingana na daktari, kadiri unavyovimbiwa, ndivyo unavyokabiliwa na shida ya gesi. Na kuvimbiwa ni hatari sana kwa mwili.

Kwa sababu "wakati gesi haijatolewa ipasavyo, inaweza kukuza maambukizi fulani ya usagaji chakula."

“Mgonjwa anapofika na kutueleza kuwa ana tatizo la gesi au kupata kinyesi kwa shida, moja kwa moja tunaomba afanyiwe vipimo ili kuona kama kuna kitu kimeziba kwenye tumbo."

Ushauri kutoka kwa daktari ili kuondoa gesi. "Lazima kwanza ujue ni muhimu sana kula kwa kiasi," anaelezea Dk Any Grah.

"Mara nyingi tunaona baadhi ya wagonjwa wetu wanaokula jioni sana, ambao hula vyakula vya wanga sana. Watu wa aina hii wako katika hatari ya kupata gesi".

Uzalishaji mkubwa wa asidi mwilini, unaweza kuchangia uzalishaji wa gesi katika mwili na kusababisha matatizo ya utumbo.

Kwa hiyo “ushuari ambalo kwa ujumla tunatoa kwa watu ni kuhakikisha kwanza tunakula kidogo jioni, kula vyakula vyenye wanga kidogo na kuepuka kunywa maziwa mengi jioni.”

Kwa sababu, anasema, kula kinyume chake hurahisisha usagaji duni wa chakula. Na asidi ni chanzo cha magonjwa mengi ya matumbo.

Pia unaweza kusoma

Imetafsiriwa na Rashid Abadalla na kuhaririwa na Ambia Hirsi