Muuguzi aliyesaidia kuzalisha watoto 10,000

w
Maelezo ya picha, Kathija anatumai kumbukumbu za siku zake za kazi zitachangamsha maisha yake ya kustaafu.

Wauguzi na wakunga ni sehemu maalum na ya lazima ya mfumo wa afya wa Kote duniani. Lakini kutokana na mahitaji makubwa ya vituo vya kutolea huduma za afya na rasilimali chache katika mataifa yanayoendelea, hawana budi kukabiliana na changamoto nyingi.

Kathija Bibi,mwanamke kutoka India alistaafu hivi majuzi alikuwa akihudumu kama muuguzi. Amepewa tunu na serikali ya Tamil Nadu kwa kufanikisha kujifungua kwa zaidi ya wanawake 10,000 kujifungua chini ya usimamizi wake.

Akikumbuka kazi yake ya uuguzi ya miaka 33, Kathija anazungumza kuhusu mabadiliko ya mitazamo kuhusu huduma ya afya ya wanawake kwa miaka mingi.

f
Maelezo ya picha, Kathija anasema uzoefu wake mwenyewe wa uzazi ulimsaidia kuelewa hofu na msisimko wa wanawake wanaokuja kujifungua.

Alizalisha watoto 10,000

Kathija mwenye umri wa miaka 60 anasema kuhusu kilele cha kazi yake, "Ninajivunia kwamba watoto 10,000 walizaliwa chini ya usimamizi wangu na hakuna hata mmoja aliyefariki wakati wa kujifungua."

Waziri wa Afya wa Jimbo Mh. Subramanian aliambia BBC kwamba Kathija hivi majuzi alipokea tuzo ya serikali kwa sababu hakuna vifo vilivyorekodiwa katika miaka yake ya utumishi.

Kwa miongo mitatu alifanya kazi katika kituo cha afya cha serikali katika jimbo la kusini la Tamil Nadu. Kiwango cha vifo vya kina mama wakati wa kujifungua kimepungua nchini India katika miaka iliyopita na sasa kinakaribia kiwango cha vifo vya wanawake wa kimataifa.

Kathija anasema ameona mabadiliko chanya katika mitazamo ya watu kuhusu kuzaliwa kwa wasichana na kuwa na watoto wachache.

Kathija alipoanza kufanya kazi mwaka wa 1990, yeye mwenyewe alikuwa mjamzito.

"Nilikuwa na ujauzito wa miezi saba... bado nilikuwa nikisaidia wanawake wengine. Nilichukua likizo ya miezi miwili baada ya kuzaliwa kwa mtoto wangu na kurudi kazini," anakumbuka Kathija.

"Ninajua jinsi wanawake wanavyokuwa na wasiwasi wakati wa kujifungua. Ndiyo maana napendelea kuwafanya wajisikie vizuri na kujiamini kwanza."

Kathija, ambaye alistaafu mwezi Juni, sasa anahisi utulivu na kuridhika kiakili.

Kliniki aliyofanyia kazi ni mji wa mashambani yapata kilomita 150 kusini mwa jiji la Chennai.

Sehemu ya upasuaji ya kliniki haina vifaa. Kwa hiyo, ikiwa matatizo yoyote yanagunduliwa kwa hali yoyote, wanawake wajawazito hutumwa mara moja kwa hospitali ya wilaya.

f

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha, Mama akiwa na binti yake mchanga

Alivyopata msukumo wa kuwa muuguzi?

Mama yake Kathija Zulaika pia alikuwa muuguzi katika kijiji hicho. Pia akawa chanzo cha msukumo kwa Kathija.

"Nilikuwa nikicheza na sindano katika utoto wangu. Nilizoea harufu ya hospitali," anakumbuka Kathija.

Kuanzia umri mdogo, alielewa umuhimu wa kazi ya mama yake katika kutoa huduma za afya kwa wanawake wa vijijini maskini na wasiojua kusoma na kuandika.

Wakati huo, hospitali za kibinafsi zilikuwa chache na wanawake kutoka asili zote walitegemea vituo vya uzazi vya serikali, ambavyo sasa vinaitwa vituo vya afya vya msingi, kwa ajili ya kujifungua.

“Wakati naanza kulikuwa na daktari mmoja, wasaidizi saba na wauguzi wengine wawili,” anasema Kathija.