Hii ni tovuti ya maandishi pekee ambayo inatumia data kidogo. Tazama toleo kuu la tovuti likijumuisha picha na video zote.
Pata maelezo zaidi kuhusu toleo hili la linalotumia kiasi kidogo cha data
Kombe la Dunia 2022: Lionel Scaloni, kocha asiye na uzoefu, alikataliwa na Maradona
Huku Lionel Messi akiwa uwanjani na Lionel Scaloni akiwa kwenye benchi, Argentina ilipata utukufu.
Wawili hao waliwaongoza albiceleste kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia mara tatu nchini Qatar 2022, ambapo ushirika kati ya wachezaji na kocha wao ulikuwa muhimu kwa ushindi.
Waarjentina hao waliwashinda Ufaransa kwa mikwaju ya penalti 3(4)-3(2), katika mojawapo ya fainali bora za Kombe la Dunia siku za hivi karibuni.
Akiwa kwenye benchi, Scaloni alijua jinsi ya kukabiliana na shinikizo la kuona Wafaransa wakisawasisa mara mbili - mara moja katika muda wa kawaida na mwingine katika muda wa ziada- na kuiongoza timu yake hadi mwisho.
Mbinu ya kocha huyo mwenye umri wa miaka 44 ilikuwa ya kushangaza: kwa dakika 80 alifanikiwa kuizuia Ufaransa, ambayo ilibidi watumie miujiza ya mfungaji mabao Kylian Mbappé kutafuta magoli ya kusawazisha.
"Scaloneta" ilihisi imevunjika, lakini katika nyakati kama zile, ambapo mchezaji anatafuta majibu, Scaloni alikuwepo.
Na Messi akiwa na Kombe la Dunia bora zaidi maishani mwake, utukufu ulimjia kocha ambaye hadi muda si mrefu alikuwa hana uzoefu, hata alidharauliwa na Diego Armando Maradona.
Mchezaji wa zamani asiye na mustakabali wazi
Scaloni alikuwa amestaafu kwa mwaka mmoja na alihisi utupu wa ndani ambao ilikuwa vigumu kupuuza.
Katika mwaka ambao sio mbali kama 2016, winga huyo wa zamani alianza kufundisha Son Caliu, kilabu ndogo katika kitongoji chake kwenye kisiwa cha Uhispania cha Mallorca, kuwafunza watoto na vijana soka.
Mwenzake Jorge Sampaoli, wakati huo aliyekuwa kocha wa Sevilla, aliona kitu ndani yake. Alimweka kufanya kazi na wale wa chini na kisha akajiunga na kikosi cha kwanza.
Lakini basi Chama cha Soka cha Argentina (AFA) kilimpigia simu Sampaoli kutafuta suluhu, kwani alikuwa kocha wa tatu katika mzunguko wa Kombe la Dunia na aliteuliwa karibu mwaka mmoja baada ya Kombe la Dunia.
Mambo kwa Argentina ya Sampaoli hayakuwa mazuri Urusi 2018, ambapo waliondolewa katika robo fainali na habari za mzozo wa ndani kati ya wachezaji na maafisa.
Iikisubiriwa kupata mbadala, AFA ilimweka Scaloni kusimamia uteuzi.
Na mustakabali wa kocha bila uzoefu kama mkurugenzi mkuu wa ufundi wa klabu au timu ya taifa itakuwa mojawapo ya mambo yasiyowezekana.
"Scaloneta"
Ukosoaji ulikuwa mkubwa kwa uteuzi wa Scaloni.
Hata Diego Armando Maradona alisema wakati huo kuwa na wakufunzi hao, Kombe la Dunia pekee ambalo Argentina wangeenda litakuwa kuendesha pikipiki, si soka.
"Scaloni ni mvulana mzuri, lakini hawezi kuelekeza trafiki," alisema mfungaji mabao huyo wa kihistoria wa Argentina.
Scaloni alisikia haya yote, lakini alichagua kutojibu. Hakuweza kubishana sana kuhusu ukosefu wake wa uzoefu, kwani miaka miwili mapema alikuwa bado akiwafundisha wavulana katika klabu mtaani mwake.
Alichagua kazi na akaionyesha kwenye Copa América ya 2021 nchini Brazil. Ilikuwa mwanzo wa 'Scaloneta', kama timu imepewa jina la utani tangu wakati huo.
Aliipeleka timu hadi fainali, dhidi ya mwenyeji na mpinzani mkuu, Brazil, alifanikiwa kuinua tena taji la bara baada ya ukame wa miaka 28.
Katika duru za kufuzu kwa Qatar 2022, Argentina ilisahau matokeo mabaya ya mizunguko iliyopita na kupata ushindi mara 11, sare sita na kupoteza sifuri.
Timu ndani na nje ya uwanja
Tofauti na ilivyotokea zamani, Messi na wenzake sasa wanatazama benchi na kuona mmoja wao.
Kushinda Kombe la Dunia tena, kama walivyofanya huko Mexico 1986, hiyo ilikuwa muhimu. Timu na mashabiki walikuwa na imani nusu na kocha wao.
Rodrigo de Paul, kiungo wa albiceleste, tayari aliangazia kutoka kabla ya fainali "usadikisho wa mambo" ambao walikuwa nao na Scaloni na jinsi walivyoikubali.
"Ikiwa sasa ni saa 10 alfajiri na Scaloni anatuambia usiku mwema, kwetu ni usiku," alisema kwa ukali.
Ingawa Qatar 2022 ilianza na kushindwa dhidi ya Saudi Arabia, mechi zilizosalia zilionyesha wazi kuwa "Scaloneta" ilikuwa na muungano mkubwa, ulioundwa kwa miaka kadhaa.
Kocha mchanga ana sheria moja tu wanapokuwa kwenye umakini: wachezaji wote lazima wakae meza moja na waweze kutazamana machoni.
Kwa wale wanaojua mafunzo ya ndani ambayo yametolewa kwa albiceleste, kama vile kocha wa zamani Lucho González, timu ya makocha imekuwa muhimu nchini Qatar 2022.
"Tuna kikosi cha kufundisha na Scaloni na wachezaji wengine wa zamani wa soka kama [Pablo] Aimar, [Roberto] Ayala na [Walter] Samuel, ambao wamepitia mengi wakiwa na jezi ya Argentina, wanajua inawakilisha nini na wana uwezo wa kuipitisha," aliiambia BBC.
"Halafu tuna kundi ambalo, ni wazi kabisa, linafanya kazi kwa furaha wanapokutana. Pia tuna mchezaji bora wa dunia, lakini timu inamfanya ajisikie vizuri na haimtegemei yeye peke. Hii imekuwa suala muhimu kwa mchakato huu."
Ilionekana kuwa na mantiki kwamba, labda baada ya michakato mingi ya Kombe la Dunia, Waajentina waliamini kweli kwamba wangeweza kushinda Kombe la Dunia.
Na wakiwa na Messi katika Kombe lake bora la Dunia na kocha wa kutumainiwa, walifanikiwa: Argentina iliinua Kombe lao la tatu la Dunia.