Jamii ya Wasomali inavyodhibiti gharama ya harusi

g

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha, Kitamaduni maharusi wa Kisomali huvaa mavazi tofauti wakati wa sherehe za harusi
Muda wa kusoma: Dakika 5

Jopo la wazee kwa ushirikiano na usimizi wa wilaya ya Xamaro, iliyopo katika eneo la Erer nchini Somalia, wametoa kakuni mpya zinazotarajiwa kuongoza jamii huko katika shughuli ya kuposa na gharama nzima ya harusi.

Uamuzi huo ambao uliafikiwa kwa pamoja na baadhi ya wakazi katika eneo hilo, unaharamisha baadhi ya vitu ambavyo vinatolewa kwa bibi harusi kabla na wakati wa harusi.

Sheikh Abdirahman Rashid, ambaye ni mkuu wa baraza la masuala ya Kiislamu katika wilaya hiyo, ameiambia BBC kwamba sababu kuu ya uamuazi huo kufanyika ni kuhusiana na maendeleo katika jamii hiyo.

'Kumekuwa na mabadiliko ya kimaendeleo kwenye sherehe ya kufunga ndoa ya kitamaduni ambayo tunaifahamu sisi, kwa msingi huo ilitubidi kukutana na kufanya uamuzi kujadiliana kuhusu aina mbaya za ndoa na mabadiliko katika jamii, hasa hapa katika wilaya ya Xamaro.'

Sheikah Abdirahman amesema kwamba mabadiliko yametokea kwenye ndoa nyingi katika miakia ya hivi maajuzi, ambayo yameweka mzigo mkubwa kwa wapenzi wanaotaka kufunga ndoa.

"Miongoni mwa vitu ambavyo tumepiga marufuku ni kupeana nguo wakati binti anafunga ndoa, kupeana miraa au mairungi na sigara – pamoja na kumchinja ngamia kabla ya siku ya harusi," alisema Sheikh Abdirahman, akiongezea kwamba, "

Mwakilishi wa familia aliyeteuliwa na familia hutwikwa jukumu la kutoa ngamia ambaye ameshakomaa anayefahamika kama Gabaati, kwa Kijiji na ngamia huyo husalia mikononi mwa jamii kwa muda uliowekwa na kisha kurejeshwa kwa mmiliki wake."

g

Chanzo cha picha, Getty Images

Hauhitaji Whatsapp
BBC Swahili sasa kwenye WhatsApp

Pata habari za kina kutoka BBC News Swahili, moja kwa moja kupitia WhatsApp.

Bonyeza hapa kujiunga

Mwisho wa Whatsapp

Utamaduni wa kutoa mahari si mgeni katika jamii hii, lakini kulingan na Sheikh Abdirahman, kuongezwa kwa masuala ya ziada kumechangia kupotea kwa tamaduni za jamii za kale.

"Ikiwa utamaduni yetu ya kale hautodumishwa, na kufanyiwa mabadiliko ya kisasa kwa kuweka mambo mapya, ingekuwa kawaida, na jamii ingenufaika kabisa, lakini kilichofanyika ni ufisadi unaokithiri na kufanya ndoa kuwa jambo gumu," alisema Sheikh, akiongezea kwamba "tamaduni nyingi ziliongenzwa kwa ule wa kale na kuchangia tatizo moja au lingine kwa vijana."

Sheikh Abdulrahman, ambaye ameelezea kile ambacho wamekipinga rasmi ni kwamba wamepiga marufuku masuala ya ziada ambayo hayakuwepo katika tamaduni ya kale.

"Tumefutilia mbali yale ya ziada, kwa mfano yaliyokuwa yakifahamika kama nyimbo, mavazi ya ziada, na mapambo, tunalenga kuhakikisha kwamba ndoa inafungwa akatika njia ya halali, na kujenga familia kihalali."

Ili kutekeleza maamuzi yaliyotolewa, Sheikh Abdirahman anasema kwamba usimamizi wa eneo utawaadhibu wote ambao wanakiuka sheria hiyo mpya.

"Kwa yule ambaye atapinga amri iliyotolewa, kuna sheria ya jinai ambayo ina adhabu ya kifungo gerezani na faini kwa mali ya atakayepatikana na hatia."

Unaweza pia kusoma:
h

Chanzo cha picha, Getty Images

Hii sio mara ya kwanza kwa uamuzi wa aina hii kutolewa kuhusiana na mfumo wa ndoa katika baadhi ya maeneo ya jimbo la Somali Regional. Amri nyingine ilitolewa awali kudhibiti tamazudi hii ila maagizo yake hayakufuatwa.

Jamii inayokaa katika mji wa Godey, ilikuwa hapo awali imekubali kupunguza gharama ya sherehe za harusi na posa. Wakazi walisema kwamba uamuazi huo ulilenga kufanya hali kuwa rahisi kwa vijana kufunga ndoa katika wakati ambapo wengi walishinda kukimu gharama ya juu ya sherehe za harusi ambazo imekuwa ikipanda katiak miaka ya hivi maajuzi.

Wanawake wanaoishi Godey ambao walihojiwa awali na BBC kupata maoni yao kuhusu gharama ya harusi, walisema kwamba hawaoni haja wala manufaa ya kufanya sherehe za kufunga ndoa kuwa nafuu.

Mmoja wa wanawake hao alisema, "Mwanamume anakuambia kuwa wewe hauna thamani yoyote kwangu," na kisha anakupa talak ama kumuoa mke mwingine, na talaka hiyo ni ya haraka sana, kisha unasalia pale kutazama mke mpya akiletwa palolikuwa nyumbani kwako. Kisha unaelezwa kwamba haufai na wala huna thamani."

Binti mwingine alisema kwamba, " Ninahisi kwamba wanaume wanalipa pesa nyingi kwa binti kwa ajili ya kumtaka kuwahudumia na kuishughulikia familia yake yote."

Mabinti wengine wanaamini kwamba hali ilikuwa ngumu katika miaka ya awali, jambo ambalo lilikuwa sababu ya talaka kidogo zilizoshuhudiwa.

Wanaume wanasemaje?

Wanaume wanaamini kwamba sherehe za ndoa zinapaswa kuwa nafuu kwa kila mtu kuwawezesha kupata fursa ya kijipatia jiko.

Ni katika eneo hilo la Somali region ambapo suala la ndoa, gharama ya harusi na hali ya Uchumi zinajadiliwa. Al-Azhar imeshaanzisha mpango wa aina hiyo kuhusu gharama ya ndoa.

Mpango huo uliowasilishwa Azhar unalenga kumaliza tamadubi mbaya na shughhli potovu katika maandalizi ya kufunga ndoa na maisha baada ya ndoa, wakiwa na matumaini kwamba kwa kufanya mambo yawe mepesi na kuzuia kuongezwa kupita kiasi kwa gharama ya shughuli hii kutakuwa nafuu kwa wengi wamaokumbana na hali ngumu ya kiuchumi hasa wenye kipato cha chini.

Aidha mpango huo utatekelezwa kwa awamu kadhaa. Ya kwamza ni shsrehe ya kufunga ndoa, ambayo inatarajiwa kuangazia masuala muhimu kabisa yalioweka kama muongozo katika dini ya kiislamu kama kusoma sura ya kwanza ya kitabu tukufu cha Q'uran na kuwaalika jamaa wa karibu kutoka familia mbili na vile vile kuhudhuriwa na wazazi wa bwana na bi harusi .

Awamu ya pili ni kuhusu maandalizi ya ndoa: 'Wanaotaka kufunga ndoa kupata mafunzo kuhusiana na maisha ya ndoa na wawili hao kukubaliana kuhusu bei ya sasa ya dhahabu, wala sio kwa misingi ya uzito wake kwa kila gramu."

Awamu ya tatu ni taratibu za kufunga ndoa ambazo huhusisha malipo ya picha zitakazopigwa siku ya harusi, kuondoa ulazima wa wanandoa kuwa na fungate na kutowalazimisha kuvalia nguo tofauti kwenye sherehe zitakazoandaliwa katika makazi ya familia hizo mbili.

Haya yote ni kupunguza gharama ya kifedha kwa vijana ambao wana matumaini ya kufunga ndoa na barafu yao wa roho.